loader
Picha

Hans Pope amekimbilia wapi? Takukuru yamsaka, yaahidi donge nono

Na Alfred Lasteck TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemtaka Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba, Zacharia Hanspope kuripoti katika ofisi za taasisi hiyo au polisi kujibu tuhuma zinazomkabili.

Aidha, Takukuru imeahidi zawadi nono kwa mwananchi yoyote yule atakayefanikisha kukamatwa kwa kiongozi huyo ambaye anadaiwa kutokomea kusikojulikana.

Mbali na Hanspope, Mkurugenzi Mtendaji na Mmiliki wa Kampuni ya Ranky Infrasture and Engineering, Franklin Lauwo naye ametakiwa kujisalimisha Takukuru ili aweze kuhojiwa.

Maagizo hayo yametolewa leo Ijumaa, jijini Dar es Salaam na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo wakati alipokutana na kuzungumza na waandishi wa habari.

Katika wito alioutoa, Mbungo alisema kuwa Hanspope kwa kushirikiana na washtakiwa wengine, Evans Aveva na Geofrey Nyange ‘Kaburu’ walitoa maelezo ya uongo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu ununuzi wa nyasi bandia (Artificial Turf) Mbungo alisema washtakiwa walisema uongo kuwa kudai kuwa walinunua nyasi bandia kutoka kwa Kampuni ya Ninah Guangzhou Trading kwa thamani ya dola za Kimarekani 40,577 (sawa na Sh milioni 92.5) na kwamba maelezo hayo yalikuwa ni ya uongo kwa maelezo kuwa bidhaa hiyo ilinunuliwa kwa dola 109,499 (Sawa na Sh milioni 249.6)

Kwa upande mwingine, Takukuru imedai kuwa, kosa la Lauwo linalomkabili ni kufanya biashara ya ukandarasi bila kusajiliwa kwenye Bodi ya Makandarasi nchini na kuongeza kuwa alifanya kazi ya ukandarasi wa ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Simba uliopo katika eneo la Bunju lililopo katika Manispaa ya Kinondoni na kulipwa zaidi ya Sh milioni 249.9.

“Tumewatafuta kwa njia mbalimbali bila mafanikio, sasa tunataka watoke walipo kusikojulikana na kuripoti Takukuru au kituo chochote cha polisi…Pia tutatoa zawadi nono kwa mwananchi atakayefanikisha kukamatwa kwa wat hao.," Bungo amenukuliwa.

Taarifa kutoka Takukuru zimebainisha kuwa Hanspope anayedaiwa kuwa na pasipoti tatu aliondoka nchini na kwenda Mombasa nchini Kenya.

“Akiwa huko Kenya inadaiwa aliondoka kwenda nchi nyingine, isipokuwa pia kuna taarifa kuwa amejificha hapa hapa nchi. Walipo kina Hanspope wanapaswa wajisalimishe, maana kuna mambo kadhaa anatakiwa kuyatolea maelezo. Tena tulibaini kuwa ana hati tatu za kusafiria zenye namba tofauti ambazo mbili ni za Tanzania na moja ya Afrika Mashariki,” alisema.

KABLA ya Yanga kukutana na As Vita ya DR. Congo ...

foto
Mwandishi: Lasteck Alfred, Dar es Salaam

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi