loader
Picha

JPM afanya Wafaransa wamwage misaada zaidi

ONGEZEKO la misaada kutoka Ufaransa kwa Tanzania kutoka wastani wa euro milioni 50 hadi 100 ili kusaidia sekta ya maji, nishati na usafi rishaji limeelezwa kuwa limetokana na taifa hilo kuridhika na mwenendo wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli inayodhibiti ufi sadi. Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na maseneta watatu wa Ufaransa wakiongozwa na Seneta Ronan Dantec walipozungumza na viongozi wa serikali, mashirika binafsi na umma, taasisi zisizo za serikali na taasisi za Kifaransa zinazofanyakazi nchini Tanzania wakiwa katika ziara ya siku saba.

Seneta Dantec alisema Tanzania ni nchi ambayo ina usalama mkubwa na amani tele na kwamba juhudi za kuifanya kuwa nchi ya uchumi wa kati wa viwanda imevutia Ufaransa kusaidia juhudi hizo za kiuchumi. Akizungumza na waandishi wa habari katika Ubalozi wa Ufaransa uliopo jijini Dar es Salaam, Seneta Dantec alisema kufuatia juhudi za Serikali katika maeneo mbalimbali, Serikali ya Ufaransa inafanya kila linalowezekana kushirikiana na Tanzania kuleta ustawi wa mataifa haya katika nyanja mbalimbali.

Alisema baada ya mkutano wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili uliofanyika Juni mwaka huu Jijini Paris, Ufaransa kati ya Makatibu wakuu wa Wizara za mambo ya nje wa mataifa hayo mawili, ujio wao nchini Tanzania umelenga kuimarisha makubaliano na kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano wao. Seneta huyo alisema pamoja na kutoa fedha hizo kwa sekta mbalimbali, pia Ufaransa itaendelea kuangalia mchango wake kufanikisha miradi ya kiuchumi yenye kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi.

Alisema Seneta Cyril Pellevat (37) na Seneta Bernard Jomier (55) na yeye wamezungumza na Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Nchi, Ofi si ya Makamu wa Rais ( Mazingira), January Makamba na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga. Seneta Dantec alisema katika mazungumzo yao waligusia miradi ambayo serikali ya Ufaransa kupitia mashirika yake inaweza kusaidia ikiwemo maendeleo endelevu ya miji kama Dar es salaam na Dodoma.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari huku akisaidiwa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier, Seneta Dantec alisema kwamba mazungumzo yao yalikuwa mazuri ukizingatia uhusiano mzuri uliopo sasa wa Tanzania na Ufaransa katika harakati za kuboresha zaidi maisha ya watu wake. Alisema lengo la ziara hiyo ni kuona namna ambavyo biashara kati ya nchi hizo mbili inavyoweza kuimarishwa zaidi hasa mazao ya kilimo na miradi mipya inayoweza kufanywa na Ufaransa hasa katika miundombinu kwenye maeneo ya utalii ikiwemo maeneo ya Kusini mwa nchi kwenye mbuga ya Selou. Maseneta hao watatembelea pia Zanzibar na kukutana na viongozi wa makampuni ya Ufaransa nchini.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi