loader
Picha

Ujenzi stendi mpya mabasi mikoani mbioni kuanza

UJENZI wa stendi mpya ya mabasi yaendayo ndani na nje ya nchi katika eneo la Mbezi Luis Jijini Dar es Salaam unatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa baada ya kumpata mkandarasi atakayejenga. Ujenzi huo unaotarajiwa kugharimu zaidi ya Sh Bilioni 50 za Tanzania, unatajwa kuwa mkubwa na wa kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati hatua ambayo pamoja na mambo mengine, itasaidia kuondoa changamoto ya muda mrefu ya kutokuwepo kwa stendi ya uhakika katika Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumzia mchakato wa ujenzi huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana alisema jana kuwa kwa sasa wapo katika tathimini za mwisho za ujenzi huo ikiwemo kumpata mkandarasi mwenye sifa atakayejenga stendi hiyo inayotarajiwa kujengwa katika viwango vya kimataifa. Alisema awali zabuni ya kumpata mkandarasi wa ujenzi huo ilitangazwa ambapo makampuni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yalijitokeza na kisha ulifanyika mchujo ili kuyapata makampuni yenye sifa yatakayofanyiwa tathimini ya kina kuipata kampuni moja itakayopewa zabuni ya ujenzi wa stendi hiyo.

“Ikumbukwe stendi hii ni ya kimataifa. Serikali imetenga fedha nyingi kuigharamia. Yapo makampuni mengi hasa kutoka nje ya nchi yameomba kazi hiyo hivyo tathmini yetu imelenga kuhakikisha kampuni inayopata kazi hiyo iwe yenye viwango vyenye uhakika ili kuepusha ujenzi usio na tija,” alisema Sipora. Kuhusu maandalizi ya ujenzi huo, Sipora alisema taratibu za ujenzi huo zimekamilika huku akigusia fi dia kwa wananchi wenye maeneo karibu na mradi kuwa tathimini hiyo na mambo mengine imewahusisha.

Hivi karibuni Waziri wa Nchi, Ofi si ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo alitembelea eneo litakalojengwa stendi hiyo na kuagiza kulipwa kwa fi dia kwa wananchi hao. Jafo alisema baadhi ya watu wanapoona miradi mikubwa kama hiyo wanapanga mikakati ya kuhujumu au kujipatia fedha kwa ufi sadi na akaonya kama wapo watu wa aina hiyo waelewe hawatabaki salama. Ujenzi wa stendi hiyo unatarajiwa kuwa suluhisho la kukosekana kwa stendi bora Dar es Salaam baada ya ile ya Ubungo inayotumika sasa kuzidiwa na abiria ikiwa haina pia barabara, majengo na vyoo.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi