loader
Juventus- Ronaldo kaonewa

Juventus- Ronaldo kaonewa

Kocha wa Juventus ya Italia, Max Allegri amesema, kama uamuzi wa video (VAR) ungetumika mshambuliaji Christiano Ronaldo (33) asingetolewa nje kwa kadi nyekundu.

Nyota huyo wa Ureno alitolewa jana usiku wakati wa mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) tangu ajiunge Juventus akitoka Real Madrid ya Hispania.

Allegri amesema, VAR ingetumika ungefanywa uamuzi sahihi na anatarajia staa wake hatafungiwa mechi nyingi.

Ronaldo alitolewa wakati kipindi cha kwanza cha mechi ya kundi H jijini Valencia Juventus wakiwa ugenini nchini Hispania.

Staa huyo alitoka uwanjani akibubujikwa machozi. Refa Felix Brych alimwonesha kadi nyekundu baada ya Ronaldo kumchezea rafu Jeison Murillo dakika ya 29 na akaonekana akimvuta nywele.

Tukio la Ronaldo kuonekana kumvuta nywele mwenzake huenda likasababisha afungiwe mechi mbili zaidi.

Staa huyo hatacheza mechi ya marudiano dhidi ya Young Boys jijini Valencia na huenda ataikosa mechi dhidi ya Manchester United Oktoba 23 Old Tafford, England.

Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA) litaamua muda wa kufungiwa staa huyo hivyo linaweza pia kutoa uamuzi utakaosababisha akose mechi ya marudiano dhidi ya Man United Novemba saba jijini Turin, Italia.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ea661d75bdf5d408a7df321692bd3d46.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi