loader
Nilijua tupo matatizoni- Mourinho

Nilijua tupo matatizoni- Mourinho

JOSE Mourinho amekiri kuwa aliona wako matatizoni wakati Phil Jones alipokwenda kupiga penalti iliyoizamisha Manchester United kulala kwa mikwaju 8-7 dh idi ya Derby County kwenye kombe la ligi juzi.

United ilikatishwa tamaa tena baada ya sare ya mabao 2 -2 katika dakika 90, baada ya Marouane Fellaini kufunga bao la kusawazisha dakika za majeruhi na kuibua matumaini kwa kikosi chake kilichomaliza mechi pungufu baada ya Sergio Romero kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 67 . B ao Fellaini lilikuja baada ya lile la Jack Marriott dakika ya 85 na ikionekana Derby anamaliza mechi hiyo kwa ushindi baada ya kuwa mbele kwa mabao 2-1 bao moja likifungwa na Harry Wilson dakika ya 59 akisawazisha lile la Juan Mata la dakika ya tatu.

Penalti zilikuwa safi kwa upande wa Derby na ilistahili, penalti 15 za kwanza hazikutoa mshindi kabla Jones kuchemka na mkwaju wake wa penalti kupanguliwa na Scott Carson. “Nimerudia nilichokisema kwenye mechi iliyopita, kwamba wao (wapinzani) kwenye chumba cha kubadilishia nguo walikuwa na imani moja kwa sababu mechi ilikuwa wazi,” Mourinho aliiambia Sky Sports.

“Tulihitaji kumaliza mechi, jambo ambalo hatukulifanya, hatuwezi kutawala mwanzoni mwa kipindi cha pili kisha baada ya kusawazisha tucheze kama vile, jambo ambalo sikulipenda.” “Niliamua kucheza wazi, lakini tukiwa 1-1 na baada ya kadi nyekundu mambo yakawa magumu.” “Tuliwa pungufu, kulikuwa na mabadiliko kidogo, timu haikutaka kufungwa na ilijaribu kupambana mpaka dakika ya mwisho.”

“Kisha wakati wa mikwaju ya penalti ukaja na mmoja alikosa, nilipoona penalti zinakwenda mpaka sita, saba, nilijua tunakwenda matatizoni na Jones, na Eric. Nilijua tupo matatizoni tena.” Kisha Mourinho kwenye mahojiano na waandishi wa habari alikanusha kwamba hakuwa akimlaumu yeyote.

“Unadhani nalaumu? sidhani,” alisema Mourinho. “Hii sio kwamba nalaumu timu, mimi ni mtu wa timu hii.” “Sidhani kama uko sahihi unaposema nalaumu, unanitaka kuchambua mchezo ama niondoke?... “Unataka niseme tulicheza vizuri? Ukweli ni kwamba wapinzani kwenye kipindi cha pili walicheza vizuri zaidi yetu na hatukuwa tayari kubadili matokeo.”

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/6a1ef6a50eed9f421fc7064eee7ee474.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: MANCHESTER, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi