loader
Messi alimchagua Ronaldo Fifa

Messi alimchagua Ronaldo Fifa

LIONEL Messi alimpigia kura Cristiano Ronaldo kwenye tuzo za mwanasoka bora wa mwaka wa Fifa.

Fifa imechapisha orodha ya manahodha wa timu za taifa na makocha kuonyesha nani alimchagua nani. Mbali na kura kutoka kwa manahodha na makocha wa timu za taifa, mwanasoka bora pia huchaguliwa na wawakilishi kutoka kwenye vyombo vya habari katika mataifa wanachama wa Fifa, ambapo kila mmoja hutakiwa kuchagua wachezaji wake watatu bora kati ya 1 0 walioteuliwa kuwania tuzo hiyo.

Luka Modric alishinda tuzo hiyo juzi akiisaidia Real Madrid kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara tatu mfululizo na kuiongoza Croatia kucheza fainali za kombe la dunia. Matokeo ya upigwaji kura, Luka Modric aliongoza kwa asilimia 29.0 5 akifuatiwa na Ronaldo (1 9.0 8) na Mohamed Salah (1 1 .2 3), Kylian Mbappe (1 0 .5 2 ), Lionel Messi (9.81), Antoine G riezmann (6.6 9), Eden Hazard (5.6 5 ), Kevin De B ruyne (3.54 ), Raphael Varane (3.45 ) na Harry Kane (0 .98) Kwa mara ya kwanza, Messi alimpigia kura Ronaldo akiwa ni mchezaji wake watatu kwenye orodha yake, lakini Ronaldo hakufanya hivyo.

B adala yake, nahodha huyo wa Ureni alimchagua mchezaji mwenzake wa zamani wa Madrid, na chaguo lake la tatu alikuwa Antoine G riezmann. Luka Modric alifanya hivyohivyo, kwa kumchagua Raphael Varane, Ronaldo na G riezmann. Raphael Varane alivutia wengi kwenye kura, pamoja na Ronaldo na Modric ambao pia walimchagua kama mchezaji wao namba moja. B eki huyo wa kati wa Ufaransa na Real Madrid alivuna kura 53, zikiwa ni nyingi kuliko beki yeyote.

Aidha, Harry Kane alishindwa kuwashawishi manahodha na makocha kumpigia kura, akipata sapoti kutoka kwa manahodha wa Bahamas, China Taipei na timu za taifa za Vanuatu ambao waote walimchagua mshambuliaji huyo wa Spurs kama mchezaji bora kwao. Kevin De B ruyne alichaguliwa namba moja na wachezaji wenzake nahodha wa Ecuador Tano B onnin na Charlie Mulgrew wa Scotland ambao wote walimchagua kiungo huyo wa Ubelgiji kama mchezaji wao bora. Nahodha wa Ufaransa Hugo Lloris hakujivunga, alichagua wachezaji wake watatu wote waliotwaa tao kombe la dunia. Namba moja Varane kisha G riezmann na Kylian Mbappe. Mohamed Salah alipata asilimia 11 .2 3 ya kura zote na kumaliza nafasi ya tatu kwa ujumla.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e824233d4835f3c26b8def6e773e02d0.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi