loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mourinho amhofia Zidane United

Mourinho amhofia Zidane United

JOSE Mo urinho ameingia katika mchecheto mkubwa kuhusu hatma ya kibarua chake katika klabu ya Manchester United, baada ya kupigiwa simu na Zinedine Zidane.

Zidane, ambaye ni mshindi wa Kombe la Dunia alipokuwa akiichezea timu ya taifa ya Ufaransa, ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya Mourinho ambaye amekalia kuti kavu katika klabu hiyo yenye maskani yake O ld Trafford. Kocha huyo alikuwa na wasiwasi na anafikiri huenda sasa wakati umefika wa kutupiwa virago kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo.

Zidane ambaye ni kocha wa zamani wa Real Madrid na anajulikana kama Zizou, alibainisha yote hayo kupitia kwa wawakilishi wake walipoulizwa kama kocha huyo ana nia na kibarua hicho. Bado inamuacha Mourinho ashawishike kuwa mabosi wa O ld Trafford wameongea na mawakala wa Zidane na wanafanya mipango ya kuondoka kwake. Kocha Mourinho ana wiki ya kutetea kibarua chake na amemshawishi Mkurugenzi Ed Woodward kuwa anaweza kumaliza mgogoro uliopo sasa.

Mourinho leo timu yake ina kibarua kigumu cha mechi ya nyumbani katika mchezo wa L igi ya Ulaya dhidi ya Valencia na wiki ijayo timu hiyo itakuwa mgeni wa Newcastle katika mchezo wa L igi Kuu ya England, ambapo atakuwa na kibarua cha kudhihirisha kazi hiyo.Kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa West Ham kimeiacha Man United katika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 10, tisa nyuma ya vinara Manchester City.

Ni mwanzo mbaya zaidi kwa klabu hiyo katika L igi Kuu baada ya mechi saba tangu mwaka 1989. G wiji la Man United G ary Neville amesema kasheshe ilianza tangu alipotimuliwa Moyes mwaka 2014. Neville aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter: “Matatizo haya yalianza wakati Man United walipomtimua Moyes na kupoteza thamani yetu yote, ambayo klabu iliijenga kwa muda mrefu sana. “Sio kocha, ni ukosefu wa suala la uongozi wa soka juu yake… ! ”

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/fd771f8d6a7d263435419da49debe0cf.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi