loader
Dstv Habarileo  Mobile
Eto’o kuzindua uwanja Dar

Eto’o kuzindua uwanja Dar

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya C astle Lager, imemualika mmoja ya wachezaji bora Afrika, Samuel Eto’o kuzindua mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira aina ya 5-A-Side utakaojengwa O ysterbay, Dar es Salaam.

Uwanja huo baada ya kukamilika utakuwa wazi kwa wananchi kucheza. Nyota huyo ambaye kwa sasa anasakata kabumbu Q atar anatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam kesho saa tisa na nusu mchana.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya C astle Lager, Pamela Kikuli alisema, nyota huyo atashiriki katika uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa uwanja maalumu wa soka linaloshirikisha wachezaji kumi (watano kila upande) maarufu kama ‘5-A-Side Soccer’ katika eneo la O ysterbay mkabala na jengo la C oco Plaza, jirani na ufukwe wa C oco. Alisema, TBL imeamua kujenga uwanja huo kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii ya Watanzania ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiwaunga mkono kibiashara.

Lakini pia akasema kuwa, lengo la kumleta nguli huyo wa soka Afrika ni kuongeza hamasa kwa wanamichezo wenye vipaji kujitokeza kushiriki katika soka hilo ambalo kwa sasa linachezwa kimataifa. Lakini pia kutoa fursa kwa watanzania ambao hawajawahi kumuona Eto’o. “Sisi sote huwa na ndoto ya kupata nafasi ya kuwaona wachezaji wa kimataifa, hasa wale wenye majina makubwa kama Eto’o.

C astle Lager ina furaha kubwa kufanya ndoto hii kuwa kweli kwetu sote kwa kutuletea mchezaji huyu mwenye hadhi ya kimataifa hapa nyumbani,” alisema Kikuli. Alifafanua kuwa, mapema mwaka huu iliendesha mashindano ya soka ya C astle Lager 5-A-Side kupitia mfumo wa bonanza na kupata mshindi ambaye alikwenda kushiriki mashindano hayo ngazi ya kimataifa Zambia.

“Tulifanya mashindano hayo na sasa tumeona kuna umuhimu kuwa na uwanja ambao utatumika bure kwa Watanzania katika kukuza vipaji vya mchezo huu, hatimaye tupate wawakilishi wazuri kimataifa kwa miaka ijayo. Mashindano haya yanafanyika kila mwaka ambapo Tanzania tumeanza mwaka huu,” alisema Kikuli.

Akizungumza katika hafla hiyo, mchezaji mkongwe wa soka nchini, Ivo Mapunda, ambaye pia ni balozi wa C astle Lager, alisema kuwa anaamini uwepo wa Eto’o nchini itakuwa chachu kwa Watanzania kushiriki katika mchezo huo.

Alisema kuwa jitihada zinazofanywa na C astle Lager katika kukuza michezo hazina budi kufuatwa na wadau wengine wa michezo katika kukuza vipaji nchini. Aliwataka wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vya jirani kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ambapo watapata fursa ya kupiga picha za kumbukumbu na Eto’o, akisisitiza kuwa nafasi kama hizo hupatikana mara chache.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a8d228d7ee25b5ada5f954e09667b914.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi