loader
Picha

Mabasi mwendokasi yaadimika

Kuna taarifa zinazodai kuwa mabasi ya mwendokasi jijini Dar es Salaam (UDART) yamegoma na kusababisha usumbufu kwa wananchi.

Leo saa mbili asubuhi kuna wananchi waliodai kuwa, walikuwa vituoni tangu saa tatu asubuhi na kwamba, hakukuwa na mabasi ya mwendokasi yaliyokuwa yakitoa huduma.

"Imekuwa kero sana, kwa hiyo nilikuwa naomba Serikali kwa jicho la tatu iangalie kama hawa watu biashara imewashinda waachieni wenye biashara hizi wanaoweza. Matajiri wapo wengi wanaotaka hizi biashara, au la warudishe hizi daladala"amesema mmoja wa wananchi aliyekuwa akisubiri usafiri Kimara.

Inadaiwa kuwa, mabasi ya UDART yamekuwa machache hivyo yaliyopo yanapita kwenye vituo vingi yakiwa yamejaa na hayasimami.

“Tumembeleza tumemwambia tunaomba utuletee gari moja tupu ameshindwa. Tunaomba ya menejimenti ya mtu wa UDART tumpigie sisi wenyewe tunajua wewe so mtu sahihi wa ku-complain (kulalamika), hatuna namba, namba zile pale zipo hamna hata moja inayopatikana, nimejaribu brother, hamna hata moja inayopatikana pale ambayo ni ya UDART” amesema mmoja wa wananchi kwenye kituo cha Kimara Korogwe.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi