loader
Picha

Jafo aagiza dawa zipatikane 98%

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amezindua mfumo wa usambazaji wa dawa, maarufu kama 'Jazia.

Ameagiza dawa zipatikane si chini ya asilimia 98 katika kila kituo cha afya wakati wasambazaji walioshinda zabuni watakapokua wameanza kazi.

Tukio la uzinduzi limekwenda sanjari na kusaini mikataba ya usambazaji kati ya Halmashauri zote za mkoa wa Dar es Salaam na washitiri (wasambazaji) ambao ni Bahari Pharmacy na Umoja Pharmaceuticals watakaosambaza dawa jijini humo.

Mfumo huo ni maalumu kusambaza dawa kuanzia pale inapoishia (inaposhindwa kufika) Bohari ya Dawa nchini (MSD) na washitiri watatakiwa kuzingatia bei za Bohari Kuu au chini yake kwa kipindi chote cha mkataba.

Imefahamika kuwa, mfumo huo hautaathiri bajeti ya serikali kuu kwa sekta ya afya, na kwamba, washitiri watakua wakilipwa kutokana na vyanzo vya vituo vya afya.

"Nimefurahishwa na jitihada zilizofanywa na kufanikisha kuwepo wa mfumo huu maana nimesikia huko nyuma hadi makampuni ya umeme yalikua yakipewa tenda ya kusambaza dawa. Hii ni kuonesha kwamba watu wamefanya vifo na matatizo ya watu kuwa uwekezaji wao. Ni hatari...," amesema Waziri Jafo.

Ameagiza zabuni zitangazwe na washitiri wapatikane katika mikoa yote kabla ya mwezi huu kuisha.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Abela Msikula

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi