loader
Picha

Waziri agoma matumizi ya mamilioni sokoni Feri

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema fedha zinachezewa kwenye soko la samaki Feri, Dar es Salaam na ameyakataa matumizi ya shilingi milioni 50.4/- kuilipa bodi inayoendesha soko hilo.

Waziri Mpina ameagiza matumizi hayo yaondolewe kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 sanjari na shilingi milioni 180/- za kuwalipa wajumbe wa bodi ya soko hilo.

"Haiwezekani ukaenda kuilipa bodi milioni 54 katika soko ambalo hata choo tuumeshindwa kuchimba."amesema akiwa sokoni hapo.

"Kwa hiyo bajeti ya mwaka wa 2018/2019 ipitiwe upya na gharama hizo zisitumike ziondolewe. Na gharama nyingine zote ambazo haizna tija ziondolewe"amesema Mpina.

Amesema, gharama za uendeshaji soko la samaki Feri hazilingani na hali halisi hivyo mikataba itapitiwa upya.

Ameagiza mikataba yote kwenye soko hilo ipitiwe upya na kama kuna matumizi mabaya ya fedha hatua zichukuliwe. Amesema, matumizi kwenye soko hilo lazima yahakikiwe kuona uhalisia wake.

Amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ahakikishe matundu 24 ya vyoo vya kisasa yanachimbwa kuanzia leo (Oktoba 10, 2018) kwenye soko hilo na hadi ifikapo Juni 30 mwakani miundombinu yote kwenye eneo hilo iwe imekarabatiwa.

Miongoni mwa maeneo yatakayokarabatiwa ni eneo la kukaushia samaki, eneo la wajasiriamali, na jokofu la kuhifadhia samaki.

Mpina amesema, hataki kusikia masuala ya mchakato, anataka kazi ya kuchimba vyoo ifanywe haraka, na kwamba, Katibu Mkuu, Mkurugenzi wa Uvuvi na Mhandisi wa wizara watajua watakapopata michoro ya vyoo hivyo.

Hivi karibuni, Rais John Magufuli aliiagiza Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam impe haraka taarifa ya mapato na matumizi ya Soko la Samaki la Feri.

Rais Magufuli alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na Manispaa ya Ilala washughulikie kero za wavuvi na wajasiriamali katika eneo hilo ukiwemo ushuru na vyoo.

Alitoa maagizo hayo kupitia kwa Katibu wake, Ngusa Samike wakati akikabidhi shilingi milioni 20 kwa Umoja wa Wavuvi Wadogo Kigamboni (UWAWAKI).

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi