loader
Picha

Kahawa ya magendo kung’oa vigogo zaidi

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amechukizwa na biashara za magendo zinazoendelea katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, hivyo amewataka viongozi wa wilaya hiyo wajipime wenyewe.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kagera, Adam Ntogha kumsimamisha kazi Ofisa wa Forodha katika mpaka wa Mulongo, Peter Mtei kwa tuhuma za kujihusisha na biashara za magendo.

Alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Kagera katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani hapa kilichofanyika mjini Bukoba.

“Biashara za magendo zinafanyika bila ya wao kuchukua hatua, mnatia aibu yaani hakuna kazi inayofanyika. Viongozi wa wilaya ya Kyerwa mjipime wenyewe, mialo mingi katika wilaya yenu inatumika kwa biashara ya magendo au butura.”

Waziri Mkuu aliongeza kuwa katika mwalo wa Mulongo ulipo kwenye eneo ambalo Tanzania inapakana na nchi za Uganda na Rwanda, biashara za magendo zinafanyika na hakuna kiongozi anayechukua hatua.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimtaka Meneja wa TRA asiwahamishe watumishi wabovu kutoka kituo kimoja cha forodha na kuwapeleka kingine kwa kuwa huko wanakowapeleka wanakwenda kuendeleza biashara za magendo na kuikosesha Serikali mapato.

Alitolea mfano mtumishi wa mamlaka hiyo, Mtei ambaye alihamishiwa kituo cha Mulongo akitokea kwenye kituo cha Mtukura kilichopo katika mpaka wa Tanzania na Uganda kwa tuhuma za kuchukua rushwa na kushirikiana na wafanyabiashara wa butura.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema mtumishi huyo tayari alishapewa barua ya uhamisho kwenda katika Kituo cha Forodha cha Rusumo miezi minne iliyopita hadi sasa hajahama na anaendelea na biashara za magendo ambapo Agosti 5, mwaka huu anadaiwa

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Kyerwa

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi