loader
Picha

RC Mbeya ataka wafanyabiashara walipe kodi

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ametangaza vita dhidi ya wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi wakidai kuathirika tangu mwaka 2007 soko la Mwanjelwa liungue.

Wafanyabiashara hao ni waliohamia Soko la Sido, lakini siku zote wanagoma kulipa kodi na kuishia kuandika barua katika ofisi ya Waziri Mkuu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Kikao cha juzi kilikuwa na ajenda mbili suala la mapato likichukua muda zaidi kujadiliwa. Mkuu huyo wa mkoa alisema wafanyabiashara hao wanaifanyia Halmashauri na serikali ya wilaya na mkoa ubabe wakiamini hawatachukuliwa hatua kwani wanawasiliana na uongozi wa juu.

Alisema jambo baya zaidi ni kuwa baadhi ya wafanyabiashara licha ya kujitapa, wamefikia hatua ya kuwachangisha fedha wenzao na kuwaahidi kuzipeleka kwa Mkuu wa Wilaya, Paul Ntinika na kwake kinyume cha sheria.

Kutokana na hali hiyo, alisema kinachofuata ni yeyote atakayekaidi kulipa kodi, kuchukuliwa hatua. Alisema wanaokwepa watatakiwa kulipa kodi yote waliyoikwepa tangu mwaka 2007.

“Ninawashwa kichwa, nawashwa mikono ninawashwa miguuu....Nataka niwaone hao wanaojiita vidume vya Mbeya. Na mkisikia kishindo ninyi msishtuke mjue tu tuko kwenye utaratibu wa kawaida wa kuwafanya watu watambue kulipa kodi ni muhimu,” alisema.

“Wapo watu wanaosema Mbeya ni pagumu. Hakuna cha ugumu. Hapa mimi nitawaonesha wagumu ni sisi tunaoshindwa kusimamia sheria. Upole wetu unatuchafua. Sasa mtaiona kazi. Nitafukua makaburi tangu mwaka 2007, “alisema.

Aliagiza wenye vibanda vya soko la Mwanjelwa walipe Sh 25,000 kwa mwezi lakini wamekataa wakitaka kulipa Sh 12,000 na alipowaita ili wazungumze, waliandika barua inayosisitizia kiwango wanachotaka huku wakituma nakala kwa Waziri Mkuu na Waziri wa Tamisemi.

Chalamila aliwaagiza wakuu wa wilaya kuongeza ukali dhidi ya wafanyabiashara wanaotaka kuwachezea kwa kukwepa serikali na kuwaonya watumishi wa umma wanaoshirikiana nao kwa maslahi yao binafsi.

Alisema hatasita kumchukulia hatua za kisheria ikiwemo kumweka rumande mfanyabiashara atakayempelekea fedha akilenga kulegezewa masharti ili awe juu ya serikali jambo alilosema wafanyabiashara wanapaswa wasahau kwake.

DC Ntinika aliahidi kutoa ushirikiano katika operesheni hiyo ya Chalamila akisema hatua ya wafanyabiashara kuichafua ofisi yake kuwa inapokea fedha wanazochangishwa wafanyabiashara sasa imevuka mipaka.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Joachim Nyambo, Mbeya

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi