loader
Picha

Wataalamu kubaini akiba mashapo ya madini

WIZARA ya Madini ipo kwenye mchakato wa kuwezesha Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania (TGS) kuwa na uwezo wa kukusanya taarifa za kina zitakazobaini akiba ya mashapo ya madini mbalimbali yaliyopo nchini.

Waziri wa wizara hiyo Angela Kairuki alisema hayo hivi karibuni kwenye warsha ya jumuiya hiyo iliyofanyika jijini Dodoma. Kairuki alisema taarifa hizo zitasaidia kuvutia zaidi na kuwarahisishia wawekezaji wanapotafuta maeneo ya utafiti wapate leseni kwenye maeneo ambayo yana taarifa na takwimu za uhakika.

Alisema kazi hiyo itaenda sambamba na kupitia upya sera ya madini ya mwaka 2009 iendane na marekebisho ya sheria ya mwaka 2010 na marekebisho yake ya mwaka 2017 pamoja na kanuni zake za mwaka 2018.

“Ili kuleta ufanisi zaidi katika ukuaji wa sekta ya madini nchini, serikali iliifuta iliyokuwa Wakala wa Ukaguzi Madini Tanzania (TMAA) na kuanzisha Tume ya Madini ambayo majukumu yake makubwa ni pamoja na kutoa vibali vya utafiti, uchimbaji, vilipuzi na ulipuaji, uchenjuaji, usafirishajc na kuishauri serikali juu ya masuala mbalimbali yanayohusu madini,” alisema.

Awali, Katibu wa TGS, Dk. Elisante Mshiu alisema kupitia umoja huo wataalamu hao wanatoa ushauri wa kitaalamu kwa serikali na taasisi zake katika kutengeneza sera zinazohusu uendelezaji endelevu wa sekta ya madini, utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi