loader
Picha

Bilionea Mo Dewji atekwa

Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji (Mo Dewji), ametekwa leo alfajiri jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa kuwa, watu wenye silaha wamemteka Mo saa 11 alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay.

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Jumanne Muliro na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa wamethibitisha kuwa Mo Dewji ametekwa.

Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa waliomteka mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo) ni wazungu wawili.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekwenda eneo la tukio na kusema kuwa, anaamini Dewji atapatikana akiwa salama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) January Makamba ameandika kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa twitter kuwa, amezungumza na baba mzazi wa Mo Dewji na amethibitisha kuwa mwanawe ametekwa.

“Nimetikiswa sana. Naamini polisi watatoa taarifa kamili. Mohammed ana familia na watoto wadogo. Tumuombee yeye na familia yake. Tusaidie kutoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwake.” ameandika Makamba.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto ameandika kwenye ukurasa wake wa twiter kuwa, ameshtushwa na kuumizwa na habari kuwa Dewji ametekwa.

“Kila mmoja wetu mwenye Taarifa zozote zinazoweza kusaidia kumwokoa asaidiane na vyombo vyetu vya dola. Mola atamsaidia MO na familia yake katika mtihani huu” ameandika Zitto. Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kuwa, tukio la kutekwa Dewji linasikitisha na kushtua.

“Aina hii ya uhalifu inaota mizizi, ana familia ana watoto ana ndugu tuendelee kumuombea kwa Allah na kila mmoja wetu kutoa taarifa yoyote atakayopata ambayo itasaidia kumpata akiwa salama Allah amlinde”ameandika Bashe.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi