loader
Picha

RC Makonda: Mabasi 20 kwa ajili ya wanafunzi yanakuja Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa mabasi 20 yameagizwa mahususi kwa ajili ya wanafunzi.

Makonda ametoa kauli hiyo mapema leo Alhamisi alipokutana na wakazi wa Kimara, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kwa lengo la kutatua kero zitokanazo na usafiri wa mwendokasi.

Hata hivyo, RC Makonda amewaonya madereva wa mabasi ya Mradi huo kuacha kuegesha magari huku abiria wakiteseka kupata huduma hiyo.

Miongoni mwa walioeleza kero ya usafiri huo wa aina yake Afrika Mashariki ni wanafunzi ambao wanasema kuwa wanachelewa shuleni, huku wafanyakazi wakisema ajira zao zipo shakani kwa kuwa hakuna usafiri za kuingia katikati ya jiji zaidi ya mabasi ya mwendokasi ambayo hudumza zao zinasuasua.

“Tunawaomba radhi sana…si kusudi la serikali. Nimeshuhudia mwenyewe..sioni sioni walemavu, wazee, wajawazito wakiweza kutumia usafiri huu. Lakini tunalishughulikia,” RC amesema huku akiwaomba wananchi hao wamruhusu akawahi kikao cha kuzungumzia kero za usafiri huo chini ya TAMISEMI.

Hata hivyo amewaonya wafanyakazi katika mradi huo kutowabughudhi abiria huku akiwataka madereva kusimama kila kituo ili abiria waweze kupanda na kuwahi sehemu zao za kuwapatia vipato.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Sauli Giliard

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi