loader
Picha

Polisi- Mo Dewji atapatikana

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema, hadi mchana huu, mfanyabiashara Mohammed Dewji Mo bado hajapatikana na juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema, tukio hilo ni la aina yake, limefanywa na raia wa kigeni na kwamba, polisi wanaendelea na oparesheni kali ya kimya kimya katika mikoa mitatu.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa polisi, Mo Dewji atapatikana mapema iwezekanavyo na ana kila sababu ya kuamini hivyo.

"Zipo taarifa mtaani kwamba ameshapatikana, wengine wanadai kwamba amepatikana kule Coco Beach, lakini taarifa kutoka meza yangu hii, na taarifa ambazo sasa ni taarifa rasmi bado hajapatikana na wahusika bado hawajakamatwa" amesema Kamanda Mambosasa.

Amewaeleza waandishi wa habari kuwa, Polisi wanafanya jitihada ili tukio hilo lisichafue taswira nzuri ya Tanzania inayotambulika kuwa ni kisiwa cha amani.

"Tunaendelea na opereshein kali kufuatia taarifa hiyo lakini bado Mo hajapatikana" amesema Mambosasa ofisini kwake.

Watu wenye silaha wamemteka Mo Dewji leo saa 11 alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa waliomteka mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo) ni wazungu wawili.

Leo asubuhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikwenda eneo la tukio na akasema, anaamini Dewji atapatikana akiwa salama.

ZIKIWA zimesalia siku chache kwa Wizara ya Nishati kuwasilisha bungeni ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi