loader
Picha

Mwuguzi amchomoa mgonjwa dripu wodini, amuuzia mwingine

MUUGUZI mmoja katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma ametoa mpya baada ya kumchomoa mgonjwa dripu ya maji na kwenda kumuuzia mgonjwa mwingine kwa bei ya Sh 5,000.

Akizungumza na gazeti hili juzi Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo ya Tunduru, Dk Wendy Robert alikiri kupokea ofisini kwake malalamiko kutoka kwa mmoja wa mwananchi ambaye alimtaja kwa jina moja la Pawasa akilalamika kitendo cha muuguzi wa zamu katika Wodi ya Wanawake kumchomoa mgonjwa dripu na kwenda kumuuzia mgonjwa mwingine.

Alisema mwananchi huyo aliingia katika wodi hiyo kwa ajili ya kumuona mgonjwa wake na kukutana na mkasa huo uliofanywa na muuguzi huyo na kwenda kutoa taarifa kwenye uongozi wa hospitali na uongozi wa hospitali hiyo ulipofuatilia uliweza kubaini kitendo hicho kilichofanywa na muuguzi huyo ambaye alidai tayari alikiuka kiapo cha Maadili ya Utumishi wa Umma katika Sekta hiyo ya Afya.

Alisema baada ya kufuatilia na kubaini ukweli wa tukio hilo ambalo lingeweza kukatisha uhai wa mgonjwa, Mganga Mkuu huyo alisema tayari ofisi yake imeanza kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na kumhoji muuguzi huyo.

Hata hivyo, Dk Wendy hakuwa tayari kutaja jina la muuguzi na mgonjwa aliyefanyiwa ukatili huo, kwa kile alichosema msemaji wake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ya Tunduru.

Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Wilaya ya Tunduru, Dk Fredrick Mabena alipohojiwa na gazeti hili alikiri kukamatwa kwa muuguzi katika hospitali hiyo ambaye alimchomoa mgonjwa aliyewekewa dripu ya maji akisumbuliwa na malaria.

Alisema muuguzi huyo baada ya kuchomoa dripu hiyo alikwenda kumuuzia mgonjwa mwingine ambaye alitakiwa apatiwe dripu kwa Sh 5,000 ambapo alidai kitendo hicho alichokifanya ni kinyume na maadili yake ikizingatiwa kiapo chake.

Alisema alipokea taarifa kutoka kwa Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Dk Wendy akimtaka afuatilie suala hilo ambalo alidai alifikishiwa na mmoja wa wananchi wa wilaya hiyo baada ya kushuhudia kitendo hicho na alipofuatilia aliweza kubaini ukweli wa tukio baada ya Muuguzi huyo kukiri mwenyewe. Alisema baada ya kukiri kosa lake kwa maandishi alipeleka taarifa hiyo kwa Mganga Mkuu wa wilaya kwa hatua zaidi za kinidhamu.

SERIKALI inafi kiria kulibadilisha Baraza la Taifa la Hifadhi na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Tunduru

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi