loader
Simba yaipumulia Yanga

Simba yaipumulia Yanga

MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba jana walifuata nyayo za watani zao Yanga baada ya kuifunga Stand United kwa mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Yanga wenyewe walicheza juzi kwenye uwanja huohuo dhidi ya timu iliyopanda daraja ya Alliance na kuibuka na ushindi kama huo na kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo nyuma ya Azam ikiwa na pointi 19.

Azam ina pointi 21. Simba kwa ushindi huo wa jana, imefikisha pointi 17 na kuwa katika nafasi ya tatu nyuma ya Yanga, ambao wenyewe wana mchezo mmoja mkononi baada ya kucheza mechi saba.

Katika mchezo huo, Simba ilifanya mashambulizi mengi katika kipindi cha kwanza na kukosa magoli kibao kabla ya kupata bao la kwanza lililofungwa na Mzambia Cletus Chama katika dakika ya 30.

Chama kabla ya kufunga bao hilo aliwahadaa mabeki wa Stand United na kuachia shuti kali lililojaa pembeni ya lango, kabla Mganda Emmanuel Okwi hajafunga bao la pili dakika chache kabla ya mapumziko.

Okwi, ambaye hilo ni bao lake la pili msimu huu, alitoka na mpira katikati ya uwanja baada ya Simba kufanikiwa kupokonya mpira kutoka kwa wachezaji wa Stand na kuupata Okwi aliyekimbia na mpira kwa kasi kabla ya kuujaza mpira wavuni baada ya kipa kujaribu kutoka langoni.

Simba walijihakikishia ushindi baada ya beki wa Stand United, Eric Mulilo kuusindikiza wavuni mpira kwa kichwa kona iliyochongwa na Ramadhani Kichuya.

Katika mechi nyingine jana, Lipuli ya Iringa ilikubali kichapo cha bao 1-0 kwenye uwanja wao wa Samora kutoka kwa Kagera Sugar huku Mbao FC ikitumia vizuri uwanja wao wa CCM Kirumba ilipoibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ad840140ce1cc5183908d4b9a37d8f32.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi