loader
Dstv Habarileo  Mobile
Arsenal, Leicester hakuna kulala

Arsenal, Leicester hakuna kulala

ARSENAL leo inashuka dimbani kukabiliana na Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England utakaofanyika kwenye Uwanja wa Emirates.

Timu hiyo inashuka uwanjani mbele ya mashabiki wake ikiwa na muendelezo mzuri wa kushinda mechi mfululizo na kuiweka katika nafasi nzuri ya kushinda katika mchezo huo wa leo usiku.

Mashabiki wa Arsenal wana kumbukumbu nzuri ya timu yao, ambayo katika mchezo wa mwisho wa ligi hiyo kabla ya kupisha mechi za kimataifa, iliibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Fulham wakati kabla ya hapo ilizifunga Watford na Everton 2-0 katika kila mchezo.

Timu hiyo kwa sasa iko chini ya kocha mpya Unai Emery, ambaye anataka kudhihirisha kuwa ni bora kwa kuiwezesha timu hiyo kumaliza ligi katika nafasi nzuri au kutwaa ubingwa, ambao wameukosa kwa miaka kadhaa sasa.

Kocha huyo mkuu anajua matatizo ya timu yake na tayari ameyarekebisha tayari kwa mchezo huo wa leo.

Kimsimamo, Arsenal kabla ya mchezo wa leo ina pointi 21 baada ya kucheza mechi nane, huku Manchester City na Liverpool zikishika nafasi ya kwanza na pili huku zikifungana kwa kila moja kuwa na pointi 23 wakati Chelsea na Tottenham zikifungana katika nafasi ya pili kwa kila moja ikiwa na pointi 21.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/390e391d02400e4948380ca3c6a3c93c.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi