loader
Barca yaikabili Inter ikimuota Messi

Barca yaikabili Inter ikimuota Messi

KUKOSEKANA kwa Lionel Messi ni pigo kubwa kwa Barcelona na kiwango cha sasa cha Inter Milan ni tishio katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya utakaozikutanisha timu hizo leo, kwa mujibu wa nahodha Mauro Icardi.

Barcelona inashuka dimbani leo bila ya kuwa na nyota wake Messi, ambaye ameshinda mara tano tuzo ya Ballon d’Or, katika mchezo huo utakaofanyika leo kwenye uwanja wao wa Camp Nou baada ya kuvunjika mkono wakati wa mchezo wa La Liga wiki iliyopita, ambao timu yao ilishinda 4-2 dhidi ya Sevilla.

Inter Milan na Barca zote kila moja imeshinda mechi zake mbili za mwanzo za hatua ya makundi za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, huku Icardi akiamini kuwa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia ya Serie A inaweza kuchuana vikali na mabingwa hao wa La liga, ambao hawatakuwa na Messi.

“Inasikitisha Messi hatakuwepo kwasababu ni vizuri kucheza dhidi ya wachezaji wakubwa kama yeye, ambaye ni mmoja wa wachezaji bora kabisa duniani, “alisema Icardi. “Tutamkosa sana na hiyo ina maana tunaweza kupambana bega kwa bega (licha ya Leo kutokuwepo) kwasababu tuna kiwango kinachotakiwa kucheza nao.”

Icardi na Inter Milan wataivaa Barcelona wakiwa wakijiamini kufuatia ushindi wao mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya watani zao AC Milan Jumapili. Icard, ambaye ni nahodha wa Inter Milan aliiibuka shujaa, shukrani kwa bao la dakika ya 92 alililofuga kwa kichwa katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa San Siro, ambako kipa wa Milan Gianluigi Donnarumma alishindwa kuzuia krosi ya Matias Vecino.

“Tulikuwa na Septemba nzuri kabla ya mapumziko yakupisha mechi za kimataifa na tulitakiwa kushinda ili kuendelea kuwepo katika njia, hivyo tumewasili Barcelona huku tukiwa na mawazo ya ushindi, kitu ambacho ni muhimu kwetu, “alisema Icardi.

Icardi pia alizungumzia hatma yake, ikiwahusisha mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, Real Madrid pamoja na Chelsea, ambao wameonesha nia ya kutaka kumsajili.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 20, ambaye angalau amefunga mabao 20 katika ligi kati ya misimu yake mitatu kati ya minne, ana tarajia kumaliza mkataba wake mwaka 2021 huku ikiripotiwa ikitakiwa kiasi cha euro milioni 110 ili kumtoa mchezaji huyo kwa klabu ngeni.

“Kumekuwa na mazungumzo mengi lakini nina furaha kubwa hapa Inter Milan, kwa sasa na baadae, na nitaendelea kuwepo hapa, “alisema Icardi. “Ofa itakapokuja tutakaa chini na kuangalia, lakini kwa sasa nina furaha kubaki hapa.”

RAIS BARCELONA

Rais wa klabu ya Barcelona, Josep Maria Bartomeu anasisitiza kuwa mabingwa hao wa La Liga bado ni washindani licha ya kutokuwa na nyota wake majeruhi, Lionel Messi. Barca wameshindwa kumuita mchezaji wao Messi kwa ajili ya mchezo huo wa makundi wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Inter Milan na atakosa pia mchezo wa El Clasico dhidi ya Real Madrid kutokana na kuvunjika mkono.

Akimzungumzia bingwa huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or, Bartomeu alisema: “Messi atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na maumivu hayo. “Bila hata ya kuwa na Leo, lakini bado tuwashindani, lakini muhimu sana ni kusonga mbele.

“Tunatakiwa kushinda kesho (leo), bila shaka hilo ndilo muhimu, na kujiandaa wenyewe. Wachezaji wako vizuri.” Ujumbe wa Bartomeu ulikuwa sawa na ule uliotolewa na Gerard Pique, ambaye alisema anaamini kuwa klabu ina uwezo wa kwenda sambamba na kutokuwepo kwa nyota huyo wa Argentina.

Kocha Ernesto Valverde huenda akamuita Ousmane Dembele au Malcolm ili kuchukua nafasi ya Messi ili kuziba pengo hilo, wakati Luis Suarez na Philippe Coutinho watakabiliwa na majukumu makubwa katika safu ya ushambuliaji.

Malcolm amecheza mara mbili katika ligi tangu alipohamia klabu hii akitokea Bordeaux wakati wa kipindi cha majira ya joto wakati Dembele alifunga mabao matatu katika mechi tisa katika kampeni hii.

Messi kwa upande wake amefunga mabao saba katika Ligi Kuu ya Hispania, La Liga, msimu huu huku akifunga mbao 12 katika mashindano yote msimu huu. Mechi zingine leo za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya: Club Brugge v Monaco PSV v Tottenham Hotspur PSG v Napoli Lokomotiv Moskva v Porto Borussia Dortmund v Atlético Madrid Liverpool v Crvena Zvezda Galatasaray v Schalke

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ecb0ef5b9b9fa6938c52393224daa6f0.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: ELONA, Hispania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi