loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pacha wafanyiwa upasuaji wakiwa tumboni

Pacha ambao bado hawajazaliwa wamefanyiwa upasuaji wa kurekebisha uti wa mgongo nchini Uingereza.

Upasuaji huo unaelezwa kuwa ni wa kwanza kufanyika nchini humo na ulihusiha madaktari 30 kutoka Hospitali ya University College.

Pacha hao walikuwa wakisumbuliwa na ugonjwa unaofahamika kitaalamu kama ‘Spina Bifida’ ambao unafanya uti wa mgongo kushindwa kukua vizuri na kuacha nafasi kati ya pingili moja ya uti wa mgongo na nyingine hivyo kuua mfumo wa fahamu wa mtoto ambao husababisha mtoto kupooza.

Upasuaji huo uliochukua muda wa dakika 90, ulihusisha mji wa mimba ‘kizazi’ cha mama na kisha kuwatibu mapacha hao. “Tulimpa mama dawa ya ganzi inayosaidia kumtuliza ila bado ni hatari kwake,” alieleza Profesa Anne David.

Kwa kawaida tatizo hili hutibiwa baada ya mtoto kuzaliwa ila kwa mapacha hawa ilibidi upasuaji ufanyike mapema ili kuokoa ukuaji wao.

RAIS wa Marekani, Donald Trump ameongeza muda wa viza za ...

foto
Mwandishi: BBC

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi