loader
Samatta amgaragaza kipa wa Liverpool

Samatta amgaragaza kipa wa Liverpool

MSHAMBULIAJI wa Klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta amefunga mabao mawili kwenye ushindi wa bao 4-2 dhidi ya Besikitas FC ya Uturuki  kwenye mchezo wa Kundi I la michuano ya Europa League uliochezwa jana kwenye uwanja wa Vodafone mjini Istanbul.

Besikitas FC iliyoongozwa na kipa aliyepo kwa mkopo kutoka Liverpool Loris Karius ilishuhudiwa ikiruhusu mabao dakika ya 23 na 63 yote yakifungwa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Samatta.

Mabao mengine ya Genk yalifungwa na viungo Dieumerci N'Dongala kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dakika ya 81 na Mpoland Jakub Piotrowski dakika ya 83 wakati kwa upande wa Besiktas, mabao yao mawili (dakika ya 74 na 86) yalifungwa na Vágner Love .

Ikumbukwe kuwa Karius alitolewa kwa mkopo na Liverpool kwenda Besikitas ya nchini Uturuki mwanzo wa msimu huu baada ya kuwa na wakati mgumu katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa Mei 26, 2018 ambapo Liverpool iliambulia kipigo cha bao 3-1 kutoka kwa Real Madrid.

Genk sasa inaongoza kundi I baada ya kufikisha pointi sita kufuatia kucheza mechi tatu, ikishinda mbili na kufungwa moja, inafuatiwa na Malmo FF yenye pointi nne sawa na Sarpsborg 08, wakati Besiktas yenye pointi tatu inashika mkia. 

Samatta jana amefikisha mechi 124 katika mashindano yote tangu amejiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na amefunga jumla ya mabao 47.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/6839b819b572b02fc9f0215112bb371c.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: Na Jacob Maganga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi