loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watumia mkojo kutengeneza matofali

Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Cape Town, Afrika Kusini wametengeneza matofali kwa kutumia mkojo wa wanaume.

Wanafunzi hao wa uhandisi, Suzanne Lambert na Vukheta Mukhari wamechanganya mkojo, mchanga, na bakteria ili kupata tofali.

“Matofali haya hutengenezwa kwa mfumo uleule ambao matumbatu ya baharini hutengenezwa,” amesema mkufunzi kutoka Chuo cha Cape Town, Dyllon Randall.

Suzanne na Vukheta wamekuwa wakivuna mkojo kutoka katika vyoo vya wanaume.

Kwa kawaida binadamu hukojoa takriban mililita 200 hadi 300 za mkojo kwa siku.

Ili tofali likamilike linahitaji lita 25 hadi 30 za mkojo hivyo kumlazimu mtu kwenda mara mia moja msalani ili kufikisha idadi ya lita zinazohitajilka.

Mchakato huo husababisha harufu kali inayotokana na mkojo lakini baada ya tofali kukamilika harufu huondoka.

“Baada ya saa 48 ya kutengeneza tofali harufu hupotea kabisa hivyo kuwa salama kwa mazingira na binadamu,” amesema Randall.

RAIS wa Marekani, Donald Trump ameongeza muda wa viza za ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi