loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kiir: Sina chembe ya hofu na ICC

RAIS Salva Kiir amesema yuko tayari kukutana na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), kama akitakiwa kwenda kujibu mashtaka kuhusu uhalifu wa kivita uliotokea wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na London School of Hygiene and Tropical Medicine inakadiria kuwa watu 382,900 wamekufa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo vilivyodumu kwa miaka mitano.

“Siogopi kwa sababu hakuna kibaya nilichofanya, kama kuna uhalifu wowote niko tayari kwenda na nitarejea,” alisema Rais Kiir wakati wa mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Citizen.

Alisema yeye si kikwazo cha amani huku akiamini mkataba wa amani kati ya serikali na makundi ya upinzani hautavunjika… “nina uhakika na ninawahakikishia wananchi kuwa nchi itakuwa na amani,” alisema.

Rais Kiir alikubali kuna maofisa wa serikali waliohusika na utakatishaji fedha za nchi hiyo na kuacha wananchi wengi wakisumbuka katika umasikini, lakini kwa sasa amejikita kuleta amani kabla ya kuchukua hatua kwa wahusika wote.

RAIS wa Marekani, Donald Trump ameongeza muda wa viza za ...

foto
Mwandishi: JUBA, Sudan Kusini

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi