loader
Kipa Leicester aelezea avyotetemeka

Kipa Leicester aelezea avyotetemeka

KIPA wa Leicester City, Kasper Schmeichel amesema kuwa ‘alitetemeka’ wakati wakipasha mwili joto kabla ya kuanza kwa mchezo walioshinda 1-0 dhidi ya Cardiff.

Huo ulikuwa mchezo wa kwanza kabisa kwa mbweha hao tangu kufa kwa mmiliki wa klabu hiyo Vichai Srivaddhanaprabha na watu wengine wanne katika ajali ya helkopta nje ya uwanja wa King Power.

Schmeichel alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kabisa kufika katika eneo la tukio ya ajali hiyo Oktoba 27.

“Nimefurahi tumefanikiwa kuondoka na pointi tatu muhimu kwa ajili yake,” alisema Dane, mwenye umri wa miaka 31, ambaye alikuwa akibubujikwa na machozi wakati wa dakika moja ya ukimya kabla ya kuanza kwa mchezo huo.

Schmeichel, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Leicester City kilichotwaa taji la Ligi Kuu katika msimu wa mwaka 2015-16, alisema:

“Leo ni siku ngumu sana. “Kufanya mazoezi ya kupasha mwili kabla ya kuanza mchezo lilikuwa jambo gumu sana. Kwa kweli dakika 10 za kwanza nilishindwa kusimama mwenyewe, nilikuwa natetemeka kweli.”

Wakati wa kupasha mwili kabla ya mchezo huo, wachezaji wa Leicester walivaa fulana yenye picha ya uso wa Srivaddhanaprabha huku ikiwa na maneno ‘The Boss’.

Wachezaji wa Leicester City na benchi la ufundi walijipanga wakizunguka katikati ya uwanja wakikaa kimya kwa dakika moja pamoja na timu ya Cardiff baada ya kuweka mashada ya maua, huku mashabiki wa pande zote wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali.

Katika mchezo huo, wachezaji wa Leicester City walionekana kucheza mchezo huo kwa hisia kali na kuwawezesha kuibuka na ushindi huo muhimu siku hiyo.

Mchezo huo ulionekana kama utakuwa sare huku mchezaji wa Cardiff, Victor Camarasa akipiga shuti lililogonga mwamba na Jamie Vardy nusura aipatie penalti Leicester wakati shuti lake lilipoonekana kama limegonga mkononi Sol Bamba.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/53706529023070060dadd7c0e7e90cb9.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi