loader
Roger Federer amzungumzia Serena

Roger Federer amzungumzia Serena

ROGER Federer anasema mkali mwenzake Serena Williams (pichani) “alienda mbali zaidi “ wakati alipombwatukia mwamuzi wakati wa fainali ya mashindano ya US Open Septemba.

Williams aliadhibiwa baada ya kumbwatukia mwamuzi na kumuita “muongo” na “mwizi” wakati akipokea kichapo kutoka kwa Mjapani Naomi Osaka.

Federer alisema kuwa tukio hilo lilichukuliwa tofauti. “Nafikiri Serena angejitoa katika mchezo”, alisema wakati akizungumza na gazeti la Sunday Times.

“Alifanya, lakini alikwenda mbali zaidi. Angeweza kujitoa mapema kabisa.”

Federer alifanya, hata hivyo, anasema hatua ya Williams kiasi fulani ilikuwa “inasameheka”. Ushindi wa Osaka wa 6-2 6-4 dhidi ya Williams Septemba 9 uligubikwa na kitendo cha Mmarekani huyo kumbwatukia mwamuzi wakati wa seti ya pili.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3aa02c7869f90a7e6da9988551ecb40d.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: NEW YORK, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi