loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ndondi kufutwa Olimpiki

Ndondi kufutwa Olimpiki

CHAMA cha Kimataifa cha Ndondi (AIBA) kiko hatarini kufungiwa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kufuatia uamuzi wake wa kumchagua Gafur Rakhimov (pichani) kuwa rais wao wa kudumu katika mkutano wao uliofanyika hapa juzi.

Ujumbe wa AIBA ulipuuzia onyo kutoka kwa IOC, ambayo ilipinga kumchagua mtu, ambaye wanamuelezea kuwa ni ‘mmoja wa waarifu wanaoongoza nchini Uzbekistan’, lakini wao wakapuuza. Lakini, mwishoni mambo yakawa tofauti wakati Rakhimov aliposhinda kwa kishindo baada ya kupata kura 86 za ndio na kumshinda mpinzani wake kutoka Kazakhstan, Serik Konakbayev.

“Tumeyapokea matokeo hayo kutoka katika Uchaguzi wa AIBA uliofanyika,” alisema msemaji wa IOC Mark Adams alipozungumza na waandishi wa habari.

“IOC imeweka wazi kuwa kuna changamoto AIBA kuhusu uamuzi, fedha, masuala ya matumzi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni, ambazo zimepigwa marufuku, pamoja na utawala bora na mambo mengine.”

Rakhimov yuko katika orodha iliyotolewa na Idara ya Fedha ya Marekani ya watu waliopigwa marufuku wakihusishwa na usafirishaji wa kimataifa wa dawa za kulevya. Marufuku hiyo imeyazuia makampuni ya Marekani kufanya biashara na mtu huyo (Rakhimov).

Hata hivyo, Rakhimov anakana kabisa kufanya baya lolote, ambapo sasa amekuwa akipambana kuhakikisha anakata rufaa ili jina lake liondolewe katika orodha hiyo ya watu waliofungiwa.

Kufungiwa kwa AIBA kuna maana kuwa chama hicho cha ndondi hakitashirikishwa kuandaa mashindano ya ndondi katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020.

Badala yake, chombo kipya kitaundwa ili kuisaidia mpango wa IOC na kuandaa mashindano ya kufuzu kwa ajili ya kushiriki Michezo ya Olimpiki 2020.

Miongoni mwa wale watakaoshirikishwa katika chombo hicho kipya, anaweza kuwa Serik Konakbayev, raia wa Kazakh, ambaye ameshindwa na Rakhimov katika uchaguzi huo mkuu.

Tayari amepanga kusafiri kwenda Lausanne wiki hii kufanya mazungumzo na IOC kulizungumzia suala hilo. Suala la AIBA ndio linatarajia kujadiliwa zaidi wakati Bodi ya Utendaji ya IOC itakapokutana jijini Tokyo kati ya Novemba 30 na Desemba 2.

“Matokeo yoyote yatakayofikiwa na Bodi ya Utendaji ya IOC, tutaendelea kufanya jitihada zote ili kuwalinda wachezaji na kuwa na mashindano ya ndondi katika Michezo ya Olimpiki Tokyo 2020.”

Lakini, IOC imekataa kuhakikisha uwepo wa mchezo wa ndondi katika michezo hiyo ya Olimpiki itakayofanyika miaka miwili baadae katika mji huo mkuu wa Japan.

Mapema, wakati akiwakilisha maelezo yake katika mkutano huo, Rakhimov mwenye umri wa miaka 67 alijaribu kuwahakikishia wajumbe kuwa uchaguo wa AIBA unaweza kuhatarisha nafasi ya mchezo wa ngumi katika Michezo ya Olimpiki 2020. “Bila shaka mchezo wa ngumi utakuwepo wakati wa Michezo ya Olimpiki Tokyo, na ile ya Paris [2024] na Los Angeles [2028], kama Michezo Olimpiki mingine ijayo,” aliwaambia.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/dbba524cfe12dd71191379b39679f6b2.jpeg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: LAUSANNE, Uswisi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi