loader
Picha

Mapato ya serikali, mishahara kupaa

SERIKALI imeeleza mapato na matumizi yake katika kipindi cha muda wa kati wa mwaka 2019/20 hadi 2021/22, huku mapato ya taifa na mishahara ya wafanyakazi ikionekana kupaa.

Waziri wa Fedha na Mpango, Dk Philip Mpango alieleza hayo jana wakati akiwalisha bungeni Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/10.

Katika hotuba yake, Dk Mpango alisema mapato ya ndani yakijumuisha mapato ya halmashauri yanakadiriwa kuongezeka hadi kufikia Sh bilioni 23,206.8 mwaka 2019/20 kutoka Sh bilioni 20,894.6 mwaka 2018/19.

Alisema ongezeko hilo linakadiriwa kukua kwa wastani wa asilimia 10.1 katika kipindi cha muda wa kati wa 2019/10 hadi mwaka 2021/22, hatua itakayowezesha makusanyo ya mapato kufikia Sh bilioni 28,113.9 mwaka 2021/22.

“Mapato ya ndani katika Pato la Taifa yanakadiriwa kuongezeka kutoka asilimia 14.6 mwaka 2019/20 hadi asilimia 14.9 mwaka 2021/22,” alisema Dk Mpango. Kuhusu mapato ya kodi, Dk Mpango aliliambia Bunge kuwa mapato hayo ya kodi yanakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 11.8 na kufikia Sh bilioni 20,124.1 mwaka 2019/10 kutoka Sh bilioni 18,000.2 mwaka 2018/19.

Alisema mapato hayo yanakadiriwa kuendelea kukua kwa wastani wa asilimia 10.1 katika kipindi cha muda wa kati (2019/20 - 2021/22) hadi kufikia Sh bilioni 24,385.4 mwaka 2021/22. “Uwiano wa mapato ya kodi na Pato la Taifa unakadiriwa kuongezeka hadi shilingi bilioni 3,082.7 mwaka 2019/2020 kutoka shilingi bilioni 2,894.4 mwaka 2018/19.

“Aidha, mapato yasiyo ya kodi yakijumuisha mapato ya halmashauri yanakadiriwa kukua kwa wastani wa asilimia 10.0 na kufikia Sh bilioni 3,728.5 mwaka 2021/22,” alisema Dk Mpango.

Akizungumzia misaada na mikopo nafuu, Dk Mpango alisema inatarajiwa kupungua kutoka Sh bilioni 3,380.2 mwaka 2019/2020 hadi Sh bilioni 3,289.9 mwaka 2021/22.

Alisema mikopo kutoka nje na ndani inatarajiwa kuwa Sh bilioni 6,913.2 mwaka 2019/20 na Sh bilioni 6,768.6 mwaka 2021/22. Matumizi ya serikali Kwa upande wa matumizi ya serikali, Dk Mpango alisema yanatarajiwa kukua hadi Sh bilioni 33,500.2 ambayo ilikuwa ni asilimia 21.1 ya Pato la Taifa mwaka 2018/19 na kukua kwa wastani wa asilimia 6.7 hadi kufikia Sh bilioni 38,172.5 mwaka 2021/22.

“Katika mwaka 2019/2020 mishahara ikijumuisha mishahara ya taasisi inakadiriwa kuwa shilingi bilioni 7,559.0 na kukadiriwa kuongezeka hadi shilingi bilioni 8,422.7 mwaka 2021/22.

“Malipo ya riba na mtaji kwa deni la ndani na nje yanakadiriwa kuwa shilingi bilioni 8,625 mwaka 2019/2020 na kuongezeka hadi shilingi bilioni 11,023.8 mwaka 2021/22,”alisema Dk Mpango.

Alisema kiasi cha kulipia bidhaa, huduma na ruzuku kinakadiriwa kuwa Sh bilioni 4,931.2 mwaka 2019/20 na kuongezeka hadi Sh bilioni 5,166.1 mwaka 2021/22. “Matumizi ya Maendeleo yanakadiriwa kuwa shilingi bilioni 12,384.4 sawa na asilimia 7.8 ya Pato la Taifa la mwaka 2019/20 na kuongezeka hadi shilingi bilioni 13,559.8 mwaka 2021/22,” alisema.

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kutowachagua wagombea uongozi katika Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Oscar Mbuza, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi