loader
Samatta ala sahani moja na Mbappe

Samatta ala sahani moja na Mbappe

HABARI ikufi kie kuwa nyota wa Tanzania na timu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta anayekula sahani moja na washambuliaji maarufu Ulaya kwa upachikaji mabao Ulaya kwa msimu huu wa ligi mbalimbali Barani humo.

Samatta amekuwa na msimu mzuri tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi hiyo maarufu kama Jupiler League, ambapo mpaka sasa anaongoza kwa ufungaji katika orodha ya wapachika mabao wa ligi hiyo akiwa na mabao 10, sawa na Landry Dimata wa Anderlecht.

Katika Ligi tano bora duniani, Hispania, Uingereza, Italia, Ujerumani na Ufaransa, ni mchezaji mmoja tu, Kylian Mbappe ndiye mwenye mabao 11 katika Ligi ya Ufaransa, hivyo kufanya tofauti kuwa ni ya bao moja dhidi ya Samatta.

Takwimu zinaonesha kuwa kwa idadi ya mabao yaliyofungwa na Samatta msimu huu ni 20 pamoja na yale ya kufuzu kwa michuano ya ligi ya Europa. Katika michezo hiyo Samatta alianza kwa kufunga bao moja dhidi ya Zulte Waregem katika mchezo wa awali na kufunga tena mabao mawili katika michezo miwili ya raundi ya tatu dhidi ya Lech Poznan.

Samatta alifunga tena mabao manne katika michezo miwili ya awali kuwania kufuzu moja kwa moja katika hatua ya makundi ya Europa dhidi ya Brondly ya Denmark. Baada ya Genk kufuzu katika hatua ya makundi, Samatta aliendelea kuwasha moto wake baada ya kupachika bao moja katika mchezo wa kwanza dhidi ya Malmo na kufunga mawili dhidi ya Besiktas ya Uturuki.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/1617a837ef5426ee444ab363c9773f34.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi