loader
Picha

Wachezaji 11 Alliance kuikosa Mtibwa

KOCHA wa muda wa timu ya Alliance FC Gilbert Daddy amethibitisha kuwa wachezaji wake 11 wataikosa mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar itakayochezwa leo kwenye uwanja wa Nyamagana.

Kwa mujibu wa Daddy, wachezaji wake wataukosa mchezo wa leo kutokana na kuwa kwenye mitihani yao ya taifa ya kumaliza kidato cha nne iliyoanza nchini kote juzi. Wachezaji hao wanasoka shule ya Sekondari Alliance.

Wachezaji hao ni Mapinduzi Balama, Rajab Kibera, Martin Kiggi, Shabaan William, Kelvin Richard, Hance Masoud, Ismail Zuma, David Richard, Godlove Mdumule, Zabona Khamis na Salim Mohamed.

Akielezea zaidi Daddy alisema wachezaji hao watajiunga na kikosi chake baada ya kumaliza mithani yao ambayo itatumia takribani wiki mbili. Aliwaomba wadau na wapenzi wa soka mkoani Mwanza waendelee kuipa sapoti timu yao ifanye vizuri katika michezo iliyosalia na kubaki Ligi Kuu. Katika msimamo wa ligi hiyo, Alliance FC inayodhaminiwa na kampuni ya Gf trucks ipo katika nafasi ya 18 ikiwa na pointi 10 baada ya michezo ya 13.

SUZAN Michael ‘Pretty Kindy’ na Rukia Juma ni miongoni mwa ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi