loader
Picha

Star Media, SOS kuwanufaisha vijana wa ‘maskani’

Watoto na vijana wanaoishi kwenye mazingira magumu nchini wanatarajiwa kunufaika na fursa za kiteknolojia ili kuendana na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Hii ni baada ya kampuni ya Star Media (T) Ltd na SOS Children’s Village Tanzania kusaini ya makubaliano kwa ajili ya kufanikisha jambo hilo.

Akizungumza baada ya kufikia makubaliano hayo kwa maandishi, Mwanasheria Mkuu wa Star Media, Justine Ndege alieleza kuwa watakaonufaika na fursa hizo ni watoto na vijana kutoka mikoa saba.

Mikoa hiyo ni pamoja na Unguja, Pemba, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Iringa.

“Moja ya mambo yatakayofanyika ni pamoja na kuwapatia nafasi vijana kujifunza kwa vitendo, ushauri, mafunzo na kukuza uelewa wa kazi na ajira kwa vijana,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa SOS Children’s Villages David Mulongo amesema ushirikiano kati ya taasisi hizi mbili utawapeleka vijana katika soko la ajira na kuwaandaa kwenye kutengeneza kesho yao.

SERIKALI inafi kiria kulibadilisha Baraza la Taifa la Hifadhi na ...

foto
Mwandishi: By JANETH MESOMAPYA

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi