loader
Picha

Shutuma za kutaka wake wa wachezaji zamvuruga Humud, kesho kuzungumza

BAADA ya timu ya KMC kutangaza rasmi kuachana na kiungo wao, Abdulharim Humud kwa shutuma za utovu wa nidhamu na kutaka wake za wachezaji wenzake, hatimaye naye amefunguka kuhusiana na hilo.

Kiungo huyo ameeleza kutopendezewa na shutuma hizo kwa kuwa zinamuharibia sifa na pia zinavuruga familia yake lakini akadai kuwa kesho majira ya saa tano asubuhi atakutana na waandishi wa habari Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ili aweke wazi kinachoendelea baina yake na timu hiyo.

Humud ambaye amesajiliwa na timu hiyo iliyopanda kushiriki Ligi Kuu msimu huu kwa kandarasi ya mwaka mmoja, zaidi ameeleza kwamba amedhalilishwa kwa namna moja ama nyingine, yeye na familia yake kwa kuwa mambo haya yamegusa masuala ya ndoa yake.

“Hii haipo sawa kwa kweli, naona kama nimedhalilishwa mimi na familia yangu. Kwa sababu haya masuala yamefika mbali, yamemfikia mama yangu na hata wakwe zangu kwa hiyo sidhani kama nitagombana na mke wangu kwa mambo haya halafu iwe ni suala la kawaida tu.

“Kwa hiyo kesho nimepanga kufanya taratibu za kukutana na waandishi wa habari, ikiwezekana pale Uwanja wa Uhuru na mimi pia nipate nafasi ya kuelezea kilichotokea na mengine mengi yaliyo nyuma ya pazia ili tuliweke sawa hili suala,” alisema Humud.

Hata hivyo, tangu kuanza kwa msimu huu, mchezaji huyo aliyewahi kukipiga Simba SC, Azam FC, Coastal Union, Sofapaka ya Kenya na hata timu ya taifa, Taifa Stars amekuwa hana wakati mzuri kwa kuwa kati ya mechi 13 ilizocheza timu hiyo mpaka sasa, amefanikiwa kucheza mechi mbili tu za awali dhidi ya JKT Tanzania na Ruvu Shooting ambazo zote ziliisha kwa sare.

      

 

SUZAN Michael ‘Pretty Kindy’ na Rukia Juma ni miongoni mwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi