loader
Picha

Wasafirishaji abiria wadaiwa kususia usafirishaji wa dagaa, samaki wa Kigoma

Usafirishaji wa dagaa na samaki aina ya migebuka kutoka Kigoma kwenda mikoa mingine imekumbwa na kizungumkuti baada ya madereva na makondakta wa mabasi ya abiria  kukataa mizigo hiyo.

Wakati hali ikiwa hivyo, kitengo cha doria na udhibiti wa rasilimali za uvuvi katika ziwa Tanganyika imekanusha kutoa agizo la kuzuia usafirishaji wa dagaa na samaki kwa ajili ya chakula au zawadi kwa ndugu kutoka mkoani Kigoma kwenda nje ya mkoa.

Afisa Uvuvi Manispaa ya Kigoma Ujiji, Azizi Daudi amekanusha kuwepo kwa utaratibu wa serikali kuzuia usafirishaji wa dagaa chini ya kilo 15 kwenda nje ya mkoa na kwamba kuanzia dagaa wenye ujazo wa kilometa 15 wanapaswa kukatiwa kibali cha usafirishaji kinachotolewa bure na manispaa yake lakini pia wasafirishaji wanapaswa kuwa na leseni ya kushughulikia rasilimali za uvuvi ikiwemo dagaa na samaki.

Daudi alisema kuwa zaidi ya wiki mbili sasa kumekuwa na opereshani ya kukamata watu wanaofanya shughuli zinazohusiana na rasilimali za uvuvi bila kufuata taratibu ambapo katika operesheni hiyo shehena ya samaki na dagaa wanaosafirishwa nje ya mkoa bila vibali walikamatwa na kupigwa faini ikiwemo magari yaliyotumika kubeba rasilimali hizo ambayo pia yalikamatwa na kupigwa faini.

"Serikali haijazuia watu wanaotaka kusafirisha dagaa au samaki chini ya kilo 15 kupeleka ndugu zao au kwa ajili ya kutumia kwa ajili ya chakula nyumbani wenye magari wameamua hizo kwa sababu wameshindwa kutafsiri kilichofanyika na kuona adhabu zilizotolewa kwa waliokamatwa na makosa wakachukuliwa hata hawa wenye kiasi kidogo pia wanahusika," alisema Daudi.

Kwa upande wake Afisa Mfawidhi wa kitengo cha doria na udhibiti wa rasilimali za uvuvi katika ziwa Tanganyika, Hamisi Beta alisema kuwa operesheni inayofanyika hausiani na ukamataji wa kiwango kidogo cha dagaa na samaki wanaosafirishwa kwani zoezi hilo limelenga kudhibiti wasafirishaji wakubwa na wafanyabiashara wasiofuata taratibu na sheria za uvuvi.

Beta alisema kuwa operesheni inahusu kudhibiti matumizi ya nyavu haramu, ukusanyaji na usafirishaji wa dagaa na samaki bila vibali na kwamba watu wanaotaka kukusanya au kusafirisha rasilimali hizo za uvuvi wanapaswa kukata leseni kwenye halmashauri inayogharimu shilingi 11,500 kwa mwaka na kupata kibali cha kukusanya na kusafirisha rasilimali hizo za uvuvi.

Emanuel James, mkazi wa Gungu, Manispaa ya Kigoma Ujiji ameieleza HabariLeo Online kuwa hili alikusudia kusafirisha dagaa kilo tano kwenda Arusha kwa kutumia basi la Kiazi Kitamu lakini alikataliwa hadi atakapokata kibali cha kusafirisha dagaa huku baadhi ya watu waliosafiri na mabasi mbalimbali wakieleza kuchukuliwa dagaa na samaki waliokuwa wakisafiri nao kwenye mabasi waliyosafiria.

SERIKALI inafi kiria kulibadilisha Baraza la Taifa la Hifadhi na ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi