loader
Picha

Mkurugenzi aeleza mvuto wa Kaliua kibiashara

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, Dk. John Pima amesema eneo hilo ni la kimkakati kibiashara na kiuchumi.

Amesema, Kaliua ni 18.8% ya eneo la mkoa wa Tabora, linafaa kwa uwekezaji kwenye sekta mbalimbali, kuna malighafi za kutosha na miundombinu rafiki.

“Tunazo fursa nyingi kwa Kaliua , nyingi sana, nyingi sana, nyingi sana, Kaliua kama tulivyosema jiografia yake inaipendelea sana Kaliua kwa maana kwamba, kwanza Kaliua inafikika kirahisi, inafikika kirahisi kwa sasa kwa maana kwamba kuna barabara kuu inayotoka Tabora kufika hapa Kaliua, nyingine inamaliziwa upande wa matengenezo kutoka Urambo kuja Kaliua kilomita 30 ndiyo zipo na mkandarasi atazimalizia wakati wowote” amesema Dk. Pima.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na timu ya kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN) iliyopo Tabora kuzitangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizopo mkoani humo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Jukwaa la Fursa za Biashara za Uwekezaji litakalofanyika kuanzia Novemba 21 hadi 23.

“Lakini tunafikika pia kwa njia ya reli, reli inatoka Dar es Salaam mpaka hapa, utoke Mwanza pia unafika moja kwa moja mpaka hapa. Lakini jambo lingine linaloifanya Kaliua iwe ni strategic point (eneo la kimkakati) ni standard gauge, ile standard gauge ambayo inajengwa itakuwa na hub kaliua, kwa hiyo standard gauge ikifika Kaliua inagawanyika inaelekea Mpanda na inaelekea pia upande wa Kigoma. Kwa hiyo chochote kitakachofanyika Kaliua kitafika popote Tanzania na nje ya nchi kwa uharaka zaidi kuliko maeneo mengine ambayo yapo katika kanda yetu hya magharibi” amesema.

Amesema Kaliua pia ina misitu ya miombo iliyopo katika sehemu ya asilimia 89 ya eneo la Mkoa wa Tabora linalotumika kwa hifadhi na kwamba, eneo hilo lina mvua nyingi na za uhakika kuliko sehemu yoyote ya Tabora hivyo ni eneo la uhakika kuwekeza katika kilimo.

“Kilimo tunafanya vizuri sana ndiyo maana umeona Kaliua imekuwa ya nne kimapato kitaifa kwa maana kwamba performance yetu inategemea kilimo na shughuli na products (bidhaa) zinazotokana na kilimo na hivyo sasa yeyote ana-invest (anayewekeza) hapa hawezi aka-regret (akajuta), hawezi akajuta” amesema Dk. Pima.

Amesema, Kaliua pia eneo bora la kuwekeza kwenye sekta ya nyama na ranchi kwa kuwa kuna ng’ombe zaidi ya 500,000 wanaolishwa vizuri kwa kuwa kuna majani mengi kutokana na wingi wa mvua.

“Kwenye mazao ya ng’ombe kuna ngozi, lakini sehemu ambayo tunahitaji sisi pia tumefanya maandalizi makubwa ni investment (uwekezaji), ni uwekezaki katka sekta ya kilimo”amesema.

UBANDIKAJI wa majina ya wakulima wote wa korosho kwenye mbao ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Kaliua

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi