loader
Picha

Amunike akuna kichwa kuiua Lesotho

KOCHA wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Emmanuel Amunike amesema atatumia muda wa kambi yake kuwasoma wapinzani wake Lesotho kabla ya kukutana Novemba 18, mwaka huu katika mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).

Taifa Stars iko kambini Afrika Kusini ikiajindaa na mchezo huo muhimu ambao utatoa nafasi ya kuamua hatma kuelekea kutafuta nafasi hiyo ya kuwakilisha nchi.

Akizungumza na gazeti hili kabla ya kuelekea kambini Afrika Kusini, Amunike alisema jambo la kwanza watatumia nafasi ya kuwasoma wapinzani na kuzungumza na wachezaji wake kitu gani kinahitaji kupata matokeo.

“Kitu cha kwanza tunachotakiwa kufanya ni kuwajua wapinzani wetu, ni timu ya aina gani ili twende kwa tahadhari na kwa kuwaheshimu, tukapambane na kutafuta matokeo mazuri,” alisema. Amunike alisema huu ni wakati muafaka kwao na wachezaji kuwafurahisha watanzania hivyo ni lazima kujipanga vizuri kuhakikisha wanaleta matumaini.

Kikosi cha Stars kinatarajiwa kukaa wiki mbili kisha kuelekea Lesotho tayari kwa mchezo huo. Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Dar es Salaam walitoka sare ya bao 1-1. Licha ya kwamba Lesotho wanashika mkia kwa pointi mbili kwenye kundi lao bado wana nafasi iwapo watafazifunga Stars na Cape Verde.

Kundi L linaongozwa na Uganda yenye pointi 10, Tanzania ikishika nafasi ya pili kwa pointi tano na Cape Verde ya nne ikiwa na pointi nne huku kila mmoja akitakiwa kutafuta matokeo mazuri katika mechi zijazo kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu. Tanzania inawania kufuzu fainali hizo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 38 tangu ilipofuzu kwa mara ya kwanza na ya mwisho ilipofanyika Lagos, Nigeria.

SUZAN Michael ‘Pretty Kindy’ na Rukia Juma ni miongoni mwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi