loader
Picha

Waziri ataja mwarobaini ajali magari ya serikali

SERIKALI imetoa onyo kali kwa viongozi mbalimbali, wakiwamo wabunge wanaowashinikiza madereva wao kuendesha kwa mwendo kasi na kuwa chanzo cha ajali zinazoongezeka za magari ya serikali. Pia imetaja hatua mbalimbali ambazo imeanza kuzichukua, ili kukomesha ajali.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Masauni Hamad Masauni alisema hayo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF) aliyetaka kujua kauli ya serikali kuhusu ongezeko la ajali za magari ya serikali.

Masauni alisema hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa kutokana na ongezeko hilo la ajali, ikiwa ni pamoja na serikali kuanza kutoa mafunzo maalumu kwa madereva wote wa serikali ili kuwafanya kuzingatia sheria za usalama barabarani.

“Tumeanza kuwapatia mafunzo maalumu madereva wa magari ya serikali na wengine ili wahakikishe kuwa wanazingatia kikamilifu sheria za usalama barabarani, ili kukomesha ajali hizi,” alisema. Alisema pamoja na hatua hizo zinazoendelea kuchukuliwa, viongozi wa serikali na wabunge, pia wanapaswa kuwa sehemu ya kampeni ya kupunguza ajali za barabarani kwa kutowahamasisha madereva wao kwenda kasi.

“Serikali inatoa onyo kwa viongozi ambao wamekuwa kiini cha ajali kwa kuwashinikiza madereva wao kwenda mwendo kasi, ni lazima viongozi wawe mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa ajali hizi za magari ya serikali zinakoma. “Serikali inaendelea kuwafuatilia viongozi wenye tabia kama hizi na watakapobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria,” alisema Naibu Waziri.

Katika maelezo yake ya swali, Sakaya alisema madereva wa magari ya serikali wamekuwa wakiendesha kwa mwendo kasi huku wakiwa wamewasha taa za magari yao na kuwafanya askari wa usalama barabarani kushindwa kuwasimamisha. Alisema hatua hiyo imekuwa kiini cha kutokea kwa ajali hizo na kusababisha vifo na majeruhi kwa watu wasio na hatia wanaosafiri na magari hayo.

Baadhi ya ajali zilizohusisha magari ya serikali ni: Julai 29, mwaka huu, watu wawili walikufa kutokana na ajali ya gari la serikali katika Kijiji cha Kalembela wilayani Chato mkoa wa Geita, ambao ni Ofisa Habari wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Shadrack Sagati na mwananchi, Semeni Kibiriti. Katika ajali hiyo watumishi wengine wanne, akiwamo dereva na naibu katibu mkuu walijeruhiwa na kulazwa hospitali.

Agosti 4, mwaka huu, kulikuwa na ajali nyingine iliyohusu gari la serikali,ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla alijeruhiwa na Ofisa Habari wa wizara hiyo, Hamza Temba alipoteza maisha. Mwezi huo huo, gari la Wizara ya Kilimo lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Shinyanga, lilipata ajali mkoani Singida na kusababisha vifo vya

SERIKALI inafi kiria kulibadilisha Baraza la Taifa la Hifadhi na ...

foto
Mwandishi: Oscar Mbuza, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi