loader
Picha

MOI yafanya upasuaji ubongo kwa darubini

KWA mara ya kwanza, Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) imefanya upasuaji wa ubongo kwa kutumia darubini ya kisasa kuondoa vivimbe kwenye mishipa ya damu kwenye ubongo kwa mgonjwa wa kiharusi.

Upasuaji huo umefanywa na madaktari bingwa wa MOI na wa Chuo Kikuu cha Weill Cornell cha Marekani. Serikali ilinunua kifaa hicho ikiwa na lengo la kuendelea kumaliza rufaa za kupeleka wagonjwa nje ya nchi, ambapo asilimia 50 ya wagonjwa hao walikuwa wanakufa na iliyobaki walipelekwa nje kwa matibabu hayo.

Jana katika taasisi hiyo waliendelea na mafunzo ya madaktari bingwa wa upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu ambako walifanya upasuaji wa kuzibua vivimbe kwenye mishipa ya damu kwenye ubongo kwa mgonjwa huyo aliyepata kiharusi.

“Upasuaji huo umefanywa kwa mara ya kwanza kwa ushirikiano na madaktari bingwa wa MOI na wa Chuo Kikuu cha Weill Cornell cha Marekani, upasuaji huo umefanywa kwa zaidi ya saa tano kwa mafanikio,” alisema Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu, Hamis Shabani.

Pia madaktari hao bingwa walifanya upasuaji wa mgongo kwa njia ya kisasa ya matundu kwa mgonjwa mwenye shida ya mgongo.

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais (Menejimenti ya Utumishi ...

foto
Mwandishi: Regina Mpogolo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi