loader
Picha

JWTZ kuanzishiwa bima ya afya

TARATIBU zinakamilishwa ambazo zitapelekwa katika mamlaka mbalimbali za serikali ili kupata ridhaa ya kuwa na Mfuko wa Bima ya Afya kwa ajili ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(- JWTZ), imeelezwa.

Hayo yamesemwa bungeni jana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi wakati akijibu swali la Mbunge wa Masasi, Rashid Chuachua (CCM) aliyetaka kujua kama serikali ina mpango wa kuwapatia wanajeshi bima ya afya.

Dk Mwinyi alisema tangu kuanzishwa kwake, JWTZ limekuwa likitumia utaratibu wa wanajeshi kupata huduma za matibabu kupitia hospitali na vituo vya afya vya jeshi kwa gharama za serikali. Alisema utaratibu huo ni kama ilivyoainishwa na Sheria ya Ulinzi wa Taifa Kanuni za 26 na 27 ya Kanuni za Majeshi ya Ulinzi Juzuu ya Kwanza (Utawala), ambazo zinabainisha kuwa huduma za matibabu kwa maofisa, askari na wategemezi wao zitagharamiwa na serikali na zitakoma pale utumishi utakapokoma.

“Ni kweli kuwa yapo malalamiko kuhusu huduma za tiba. Malalamiko hayo yanatokana na huduma kutokidhi mahitaji halisi kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha kugharamia dawa na vifaa tiba katika hospitali za jeshi.

Hivyo, kutokana na upungufu na changamoto zilizopo, kumeonekana umuhimu wa kuwa na Mfuko wa Bima ya Afya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania,” alisema. Katika swali la nyongeza, Mbunge wa Ulanga Mashariki, Goodluck Mlinga (CCM) alitaka kujua kama serikali ina mpango wa haraka wa kusaidia familia za wanajeshi wanaoishi nje ya makambi na kupata shida ya kupata matibabu kutokana na kuwa mbali na hospitali za jeshi zilizo ndani ya makambi.

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais (Menejimenti ya Utumishi ...

foto
Mwandishi: Oscar Mbuza,

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi