loader
Picha

Serikali yatoa mafunzo ya umahiri kwa mabaharia

KATIKA kuimarisha usalama wa usafiri wa majini, serikali imekuwa ikiendesha mafunzo ya vyeti vya umahiri kwa mabaharia, Bunge limeelezwa. Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Atashasta Nditiye wakati akijibu swali la Mbunge wa Nungwi, Yussu Haji Khamis(CUF). Katika swali lake, mbunge huyo alihoji mkakati endelevu wa serikali wa kuhakikisha usafiri wa majini ni salama kwa maisha ya Watanzania.

Katika majibu yake, Naibu Waziri Nditiye alisema serikali inatambua changamoto zilizopo katika usafiri wa majini nchini, katika kuhakikisha kuwa changamoto hizo zinatatuliwa. Alisema serikali imendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha na kuimarisha usalama wa usafiri huo wa majini kwa kutunga sheria na kanuni zinazosimamia usalama wa usafiri wa majini. “Aidha, katika kuimarisha usalama wa usafiri wa majini, serikali pia imekuwa ikiendesha mafunzo ya vyeti vya umahiri kwa mabaharia.

Mafunzo hayo yanatolewa katika viwango vya kimataifa na yanatambuliwa na Shirika la Bahari Duniani (IMO) kupitia Mkataba wa utoaji wa vyeti kwa mabaharia,” alisema. Alisema katika kuimarisha usimamizi na udhibiti wa usafiri wa majini nchini, serikali ilitunga Sheria Namba 14 ya Mwaka 2017 na kupitia sheria hiyo, serikali ilianzisha shirika maalum la udhibiti wa usalama wa vyombo vya majini.

Alisema sambamba na hilo, serikali pia imeweka utaratibu wa ukaguzi na utoaji wa vyeti kwa vyombo vya majini zikiwemo meli. “Ukaguzi huu hufanyika angalau mara mbili kwa mwaka, lengo likiwa ni kujiridhisha na usalama wa vyombo hivyo katika utoaji huduma ya usafiri majini,” alisema.

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais (Menejimenti ya Utumishi ...

foto
Mwandishi: Oscar Mbuza,

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi