loader
Picha

Watalii kuongezeka Tarangire

MHIFADHI wa utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Neema Philipo amesema idadi ya watalii wa ndani mwaka 2017-2018 inatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 10 ikiwa ni zaidi ya watalii 76,829 waliokwishatembelea hifadhi hiyo kufi kia Julai mwaka jana, kutokana jitihada na mipango madhubuti inayofanyika kutangaza utalii wa ndani.

Akizungumza na gazeti hili ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Philipo alisema idadi hiyo itaongezeka kwa asilimia 10 au zaidi ukilinganisha na mwaka 2016-2017 ambayo hadi kufikia Julai mwaka jana, idadi ya watalii waliotembelea walikuwa 76,995 tu. Alisema mwaka 2014- 2015 waliotembelea Hifadhi ya Tarangire walikuwa 49,200 ambao mwaka uliofuta 2015-2016 waliongezeka na kufika 64,022.

Alisema ongezeko hilo litaongezeka kutokana jitihada zilizofanywa na zinazofanywa na timu ya idara ya utalii ya hifadhi hiyo kuhakikisha wanapita shule, vyuo, taasisi za watu binafsi na serikali, kwenye mikutano ya vijiji, makongamano na mikutano na kutangaza umuhimu wa kutembelea vivutio.

“Tukishapokelewa kwenye sehemu hizo kwa lengo la kutangaza utalii, tunafundisha kwani wengi hawafahamu utalii sio kuona wanyama tu, uko mwingi sana, pia tunajitajidi kubadilisha mtazamo wa Watanzania kwamba kutembelea hifadhi ni anasa,”alisema. Alisema barabara zilizopo kwenye hifadhi hiyo zinapitika kwa magari ya kawaida ya abiria kama Toyota Coaster, Hiace, mabasi na magari mengine madogo.

Philipo alitaja vivutio vinavyopatikana kwenye hifadhi hiyo kuwa ni makundi makubwa ya tembo, aina tofauti za wanyama wakubwa, idadi kubwa ya miti ya mibuyu, chatu wanaopanda Mto Tarangire na mabwawa. Alitaja pia bidhaa za utalii kuwa ni kuangalia wanyama, utalii wa kutembea kwa miguu, utalii wa kuruka na puto, utalii wa kupiga picha, kupiga kambi, utalii wa usiku na utalii wa kula porini.

Hifadhi ya Tarangire inatekeleza mpango wa miradi mbalimbali ya ujirani mwema kwenye maeneo ya vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo. Mhifadhi wa Idara ya Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Tarangire, Heriel Masaki alisema hifadhi hiyo inapakana na vijiji 46 na 23 kati ya hivyo vinapakana moja kwa moja. Vijiji vingine 23 havipakani moja kwa moja isipokuwa vipo kwenye Mfumo wa Ikolojia wa Hifadhi za Manyara na Tarangire.

Alitaja baadhi ya miradi inayotekelezwa katika baadhi ya vijiji ili kuimarisha ujirani mwema mwaka 2015-2016 kuwa ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha Gijedabou kilichopo Wilaya ya Babati uliogharimu Sh milioni 65. Alitaja miradi mingine ni ujenzi wa jengo la utawala la Shule ya Sekondari ya Emboret wilayani Simanjiro uliotumia Sh 89,221,050 na ujenzi wa madarasa mawili ya Sekondari ya Mbugwe, Simanjiro uliogharimu Sh milioni 44.

Kilombero yapewa mil 700/- kuboresha vituo vya afya Na Mwandishi Wetu, Chunya KAMPUNI ya Tanzania Leaf Tobacco Limited (TLTC), imepongezwa kutokana na mchango wake wa kiuchumi na kijamii katika miongo mitano ya kazi zake nchini. Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary Mahundi amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa sherehe za kutimiza miaka 50 ya TLTC. Mkuu huyo wa wilaya amesema kampuni hiyo imebadili maisha ya wakulima wengi wa tumbaku, familia za waajiriwa na taifa kwa ujumla kutokana na mchango wake wa kiuchumi.

“Nawapongeza TLTC kwa kujenga ushirikiano wa muda mrefu na wakulima wadogo pamoja na serikali, jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi,” alisema. Aidha, alisema kampuni hiyo ya tumbaku pia imechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya jamii kwa ufadhili wake wa kifedha kupitia ushiriki katika miradi ya kijamii. Kauli hiyo ya mkuu wa wilaya iliungwa mkono na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania, Dk Julius Ningu aliyeipongeza kampuni hiyo kwa kazi nzuri.

Akizungumza mkoani Tabora wakati wa sherehe hizo za kutimiza 50 ya TLTC, Dk Ningu alisema katika umri huo, wakulima wadogo pia walinufaika kwa kiasi kikubwa kwa kulima na kuuza bidhaa hiyo kwa kampuni hiyo. Na John Nditi, Morogoro HALMASHAURI ya Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro imepatiwa Sh milioni 700 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kuboresha vituo vya afya na kununulia vifaa tiba.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, David Ligazio wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika hivi karibuni mjini Ifakara. Ligazio alisema serikali inaendelea kutoa huduma nzuri kwa wananchi katika halmashauri hiyo na moja ya jukumu kubwa ni kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake. Mwenyekiti huyo alisema katika fedha hizo Sh milioni 500 zimetolewa kwa ajili ya kuboresha vituo vya afya wakati Sh milioni 200 zimeelekezwa katika upatikanaji wa vifaa tiba.

“Fedha hizi zimetolewa mwaka huu na nyingine mwaka jana ambazo zilipelekwa katika maboresho ya Kituo cha Afya cha Mlimba,” alisema. Alisema fedha hizo Sh milioni 700 zipo nje ya zile zinazopelekwa kila baada ya miezi mitatu katika vituo vya afya. Mwenyekiti wa halmashauri hiyo alisema kwa sasa halmashauri ina vituo vya afya vinne ambavyo ni Mlimba, Mngeta, Mang’ula na Mgudeni.

Katika hatua nyingine, baraza hilo limefikia uamuzi wa kumtimua kazi mmoja wa dereva wa halmashauri hiyo (jina limehifadhiwa), baada ya kubainika kuwa alitumia vyeti feki wakati wa ajira yake na hiyo imetokana na uhakiki ulioendeshwa na serikali hivi karibuni. Kaimu

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais (Menejimenti ya Utumishi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi