loader
Picha

Kilombero yapewa mil 700/- kuboresha vituo vya afya

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro imepatiwa Sh milioni 700 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kuboresha vituo vya afya na kununulia vifaa tiba. Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, David Ligazio wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika hivi karibuni mjini Ifakara.

Ligazio alisema serikali inaendelea kutoa huduma nzuri kwa wananchi katika halmashauri hiyo na moja ya jukumu kubwa ni kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake. Mwenyekiti huyo alisema katika fedha hizo Sh milioni 500 zimetolewa kwa ajili ya kuboresha vituo vya afya wakati Sh milioni 200 zimeelekezwa katika upatikanaji wa vifaa tiba.

“Fedha hizi zimetolewa mwaka huu na nyingine mwaka jana ambazo zilipelekwa katika maboresho ya Kituo cha Afya cha Mlimba,” alisema. Alisema fedha hizo Sh milioni 700 zipo nje ya zile zinazopelekwa kila baada ya miezi mitatu katika vituo vya afya.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo alisema kwa sasa halmashauri ina vituo vya afya vinne ambavyo ni Mlimba, Mngeta, Mang’ula na Mgudeni. Katika hatua nyingine, baraza hilo limefikia uamuzi wa kumtimua kazi mmoja wa dereva wa halmashauri hiyo (jina limehifadhiwa), baada ya kubainika kuwa alitumia vyeti feki wakati wa ajira yake na hiyo imetokana na uhakiki ulioendeshwa na serikali hivi karibuni.

SERIKALI inafi kiria kulibadilisha Baraza la Taifa la Hifadhi na ...

foto
Mwandishi: John Nditi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi