loader
Picha

DC aipongeza kampuni ya tumbaku kuchangia uchumi

KAMPUNI ya Tanzania Leaf Tobacco Limited (TLTC), imepongezwa kutokana na mchango wake wa kiuchumi na kijamii katika miongo mitano ya kazi zake nchini. Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary Mahundi amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa sherehe za kutimiza miaka 50 ya TLTC.

Mkuu huyo wa wilaya amesema kampuni hiyo imebadili maisha ya wakulima wengi wa tumbaku, familia za waajiriwa na taifa kwa ujumla kutokana na mchango wake wa kiuchumi. “Nawapongeza TLTC kwa kujenga ushirikiano wa muda mrefu na wakulima wadogo pamoja na serikali, jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi,” alisema.

Aidha, alisema kampuni hiyo ya tumbaku pia imechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya jamii kwa ufadhili wake wa kifedha kupitia ushiriki katika miradi ya kijamii. Kauli hiyo ya mkuu wa wilaya iliungwa mkono na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania, Dk Julius Ningu aliyeipongeza kampuni hiyo kwa kazi nzuri.

Akizungumza mkoani Tabora wakati wa sherehe hizo za kutimiza 50 ya TLTC, Dk Ningu alisema katika umri huo, wakulima wadogo pia walinufaika kwa kiasi kikubwa kwa kulima na kuuza bidhaa hiyo kwa kampuni hiyo.

SERIKALI inafi kiria kulibadilisha Baraza la Taifa la Hifadhi na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi