loader
Picha

Vodacom, CBA zaja na Shinda na M-Pawa

BENKI ya Biashara Afrika (CBA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Vodacom, imezindua huduma ya ‘Shinda na M-Pawa’ itakalomwezesha mteja kuhifadhi hela na kukopa kwa urahisi.

Akizundua huduma hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mwakilishi wa Mkurugenzi katika benki hiyo, Julius Konyani alisema CBA imekuja na 'Shinda na M-Pawa' baada ya kuona watanzania wengi hawapo kwenye sekta rasmi ya kibenki.

Alisema huduma hiyo itamwezesha mteja kuhifadhi hela zake na kukopa baada ya kuhifadhi kiasi cha pesa kwenye huduma ya M-Pawa inayotolewa na Vodacom. “Mteja akihifadhi hela anapata riba. Na atakapowekeza ataweza kukopa kwenye M-Pawa muda wowote.

Mteja anaweza kukopa kuanzia sh. 1,000 hadi sh. milioni tano,” alisema. Alisema CBA ilitengeneza teknolojia na kuiweka kwenye M-Pawa, baada ya kuanzisha huduma hiyo miaka mitatu iliyopita na sasa wana wateja laki saba.

Alisema kwenye kampeni hiyo wana lengo la kuwazawadia wateja wanaotumia M-Pawa, watakuwa na uwezo wa kujishindia mara mbili ya amana zao. Alisema kila wiki watawazawadia wateja 200 hivyo kwa wiki sita watakuwa wateja 1200.

“Kwa droo ya wiki tutakuwa na wateja 15 waliokopa na kurejesha mapema watazawadiwa sh. 100,000. Kwa jumla ya wiki sita watakuwa wamewazawadia wateja 90,” alisema. Konyani alisema wiki ya mwisho wateja watano wana nafasi ya kujishindia bajaji moja na mteja mmoja atajishindia Sh. milioni 10.

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais (Menejimenti ya Utumishi ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi