loader
Picha

China, Urusi kuimarisha uhusiano wa kisiasa

CHINA na Urusi zimekubaliana kuendeleza, kuimarisha uhusiano wao wa kisiasa na kimkakati pamoja na kupanua ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara baina yao.

Makubaliano hayo yalifikiwa hivi karibuni kati ya Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang na mwenzake wa Urusi Dmitry Medvedev wakati wakiendesha kwa pamoja mkutano wa kawaida wa wakuu wa serikali wa China na Urusi mjini Beijing.

Imeelezwa kuwa mkutano huo ni wa aina yake na wa kipekee tangu nchi hizo ziunde serikali mpya, lakini pia una umuhimu mkubwa kwa kuwa unakuwa kama daraja linalounganisha zama zilizopita na zama zijazo.

Li alisema kuwa China na Urusi ni majirani wakubwa katika ukanda huo, hivyo kila mmoja ana fursa muhimu za kimaendeleo. “China iko tayari kufanya kazi na Urusi ili kuimarisha uhusiano wetu wa kisiasa na kuaminiana, kupanua kila aina ya ushirikiano tulionao pamoja na kuchangia kwa pamoja amani, utulivu na maendeleo duniani,” alisema Li.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu huyo wa China, ukubwa wa ushirikiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili utaongezeka kwa zaidi ya dola za Marekani bilioni 100 za Marekani kufikia mwisho wa mwaka.

Li alitoa wito kwa pande zote mbili kuboresha mazingira ya kibiashara, kuongeza uwekezaji, ushirikiano katika kilimo, kuinua biashara ya mipakani kimtandao pamoja na kuimarisha ushirikiano kwenye maeneo ya uvumbuzi hususani sayansi, teknolojia na utafiti.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Urusi, Medvedev alizitaka pande zote mbili kuimarisha uhusiano wao kwenye biashara ya mtandao, uvumbuzi, kilimo, nishati, nishati ya nyuklia na usafirishaji.

Medvedev alitoa wito kwa serikali za nchi zote mbili kusaidia ushirikiano kati viwanda vidogo na vya kati katika nchi zao pamoja kushirikiana katika mambo ya mafuta na gesi asilia.

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais (Menejimenti ya Utumishi ...

foto
Mwandishi: BEIJING, China

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi