loader
Picha

JPM afanya afanya mabadiliko, Waitara aula, Mwijage na Tizeba 'OUT'

MAWAZIRI Charles Mwijage wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Dk Charles Tizeba wa Kilimo, wametemwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri waliyofanywa na Rais John Magufuli leo  jioni.

Rais Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri kwa kuteua mawaziri wawili na Naibu Mawaziri wanne.

 

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kuwa Waziri wa Kilimo kuchukua nafasi ya Dk Tizeba.

Aidha, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Joseph Kakunda kuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, akimbadili Mwijage.

 

Taarifa hiyo ya Ikulu iliongeza kuwa Rais Magufuli amemteua Constantine Kanyasu kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii. Kanyasu ambaye ni Mbunge wa Geita Mjini mkoani Geita, anachukua nafasi ya Hasunga.

 

Aidha, Rais Magufuli amemteua Dk Mary Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kabla ya uteuzi huo, Dk Mwanjelwa alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

MAMLAKA ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi