loader
Neymar amliza Suarez baada ya kuitungua Uruguay

Neymar amliza Suarez baada ya kuitungua Uruguay

PENALTI ya utata ya Neymar iliiwezesha timu ya taifa ya Brazil kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uruguay katika mchezo mkali wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Emirates unaomilikiwa na Arsenal ya Ligi Kuu England.

Mshambuliaji huyo nyota wa klabu ya Ufaransa ya Paris St-Germain (PSG), alifunga kwa penalti baada ya Diego Laxalt kumfanyia rafu mchezaji wa Brazil anayechezea klabu ya England ya Manchester City, Danilo.

Neymar alifanyiwa rafu nyingi, huku Uruguay ikipata kadi sita za njano kutoka kwa mwamuzi Craig Pawson. Uruguay sasa imeshindwa kuifunga timu hiyo ya Amerika ya Kusini katika mechi 10 walizokutana.

Timu zote zilipanga vikosi kabambe, huku Brazil ikiwachezesha wachezaji wa Liverpool, Alisson na Roberto Firmino, wakati mchezaji wa Everton, Richarlison akianzia benchi.

Lucas Torreira wa Arsenal alicheza kwenye uwanja wao wa nyumbani, na ni miongoni mwa wachezaji waliomchezea rafu Neymar, na kupata kadi ya njano.

Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez alifanya jitihada, na alikaribia kufunga lakini shuti lake liliokolewa na Alisson.

Brazil inajiandaa kwa ajili ya mashindano ya Copa Amerika 2019 yatakayofanyika kwenye ardhi yao na wataendelea na maandalizi watakapocheza dhidi ya Cameroon Jumanne.

Uruguay itakwenda Paris, Ufaransa wiki ijayo kucheza na mabingwa wa Dunia Ufaransa, ambao juzi waliofungwa na kuhitimisha ushindi wa mechi 15 mfululizo

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9a59639364e0a943513cbe198c5b2e9f.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: Mashirika, London

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi