loader
Picha

FIlamu ya Widows: Ogopa sana kisasi cha mwanamke

NOVEMBA 16 kwa wenzetu wa majuu wamepata bahati ya kuangalia kwa undani sinema ya Widow ambapo steringi wetu Viola Davis anaongoza kundi la wajane kutengeneza kisasi dhidi ya wakora waliokuwa wakishirikiana nao.

Katika simulizi hili la Steve McQueen ikiwa ni filamu yake ya kwanza baada ya kutoa ‘12 Years a Slave’wanawake hawa wameweza kuleta burudani kubwa ambayo ni nadra sana kuona katika sinema za visasi. 

Unaweza kujiuliza je, Widows ni sinema iliyotulia kabisa. Kwa kuangalia maandishi mbalimbali ya watu walioiangalia hasa kwenye tamasha la Toronto, unaona kwamba hii sinema ni babu kubwa kutoka kwa mtu ambaye akitoa visa vyake ni hatari tupu, Steve Mc- Queen, ambaye pia amedarekti Hunger na Shame .

Ni sinema ya aksheni, yenye vionjo vitamu vya kufurahisha ikiwamo mapenzi na dhana nzima ya mali fedha na fedheha. Sinema hii ambayo inaonesha namna watu wanavyoweza kuamua kutenda mambo yao mkidhani hawawezi, imetengenezwa vyema zaidi kwa kuangalia mpaka mambo ya kibaguzi na kudhalilishana.

Darekta katika kupambanua haya, amekuwa akifanya katika kila kipande cha simulizi na katika hali hiyo kutengeneza aina ya chachandu ambayo lazima uile kwa raha.

Kwa wale ambao wanapenda kuzungumzia ubora, sinema hii ya wanawake wakiwa wanawapeleka puta wanaume ni moja ya sinema bora. McQueen na mwandishi wa Gone Girl anayekwenda kwa jina la Gillian Flynn, wametengeneza Widows kwa kuzingatia tamthilia ya mwaka 1983 na 1985 zilizoandikwa na Lynda La Plant, ambaye anatambulika kwa kazi njema kwenye tamthilia ya uingereza ya Prime Suspect. Darekta huyu katika dakika chache anakubadilikia na kukufanya ujisikie kabisa kwamba na wewe uko msambweni.

Ndani ya “Widows,” niseme kidogo , masuala ya ndoa yanaonekana kuwa ni masuala yanayolipa hasa kutokana na kila mmoja kujazia pale ambapo mwenzake hawezi au hafanyi. Simulizi linaloga pale unapojua kwamba wanawake wote hawa waliolewa na wahalifu halafu hawakuwa wanajua kwamba waume zao ni wahalifu.

Shida inaanzia pale ambapo kazi moja inaingia mdudu, na Harry Rawlings (Liam Neeson) aliyeongoza kundi hilo la wezi kujikuta wanakaangwa na kikosi maalumu SWAT asitoke mtu.

Mke wa Harry, Veronica (Davis), akiwa amejawa na majonzi anakutana na kigingi kwamba anatakiwa kulipa dola milioni 2 anazodaiwa mume wake na ana mwezi mmoja kulipa fedha hizo. Pamoja na kuwa na fedha , hiyo fedha ilikuwa kali na Veronica alikuwa hana. Akiwa katika hekaheka ya fikira anagundua mpango wa wizi uliotengenezwa na mume wake na ndipo anapojua maisha ya mume wake na biashara zake. Akiwa anajua wanawake wengine walivyofanywa anawaita na kuwoangoza kufanya uhalifu na katika njia hiyo kulipiza kisasi.

Anapata msaada wa Linda (Michelle Rodriguez), mdada wa mtoto mmoja ambaye deni la mume wake lilifilisi biashara yake na Alice (Elizabeth Debicki), msichana mrembo aliyegeuka kuwa msindikizaji bila kupenda. Veronica anapambana na kwa msaada wa wenzake akina Jamal (Brian Tyree Henry), Jatemme (Daniel Kaluuya) , mwanasiasa wa Chicago , Tom Mulligan (Robert Duvall) na mtoto wake Jack (Colin Farrell) waliotaka milioni 2,watu hawa washenzi katika siasa kwa rushwa na kwa kila kitu wanaona nyota mchana. Ingawa Simulizi la hadithi hii ni gumu kidogo lakini kimsingi sinema hii unaipata katika dunia ya leo, dunia ya udanganyifu, rushwa na tamaa ya maisha.

Unapoitazama Widows ni kama unatazama kwa namna fulani mambo yanavyostahili kubadilika na si kuwa kama kawaida. Ni sinema ambayo inaangalia hivi kunatokea nini katika jamii zetu wanadamu. Sinema hii imejaa vurugu, lugha ya maudhi na vipande vya kutazamwa na wakubwa imepewa daraja Rkungonoka ni sinema iliyopewa daraja la R inatembea kwa dakika 128.

Kutoka huku Goba Kibululu, Kwa John Luwanda unaweza kunipata katika sms 0713176669 au msimbebeda@gmail.com aksanteni sana jumapili njema na wiki njema.

 

HIVI karibuni Wizara ya Nchi Ofi ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi