loader
Picha

Katibu Mkuu UN amteua Mtanzania kuongoza UNEP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN),António Guterres amemtea Mtanzania Joyce Msuya kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira (UNEP).

Kwa mujibu wa taarifa za shirika hilo jijini Nairobi, uteuzi huo umefanyia leo Jumatano (Novemba 21, 2018) kujaza pengo lililoachwa na Mkurugenzi Erik Solheim ambaye alitangaza kujiuzulu jana Jumanne baada ya kuhusishwa na ubadhirifu wa dola za Kimarekani 500,000 (takribani Shilingi bilioni 1.2) katika kipindi cha miezi 22 pekee.

Kabla ya kuteuliwa kukaimu nafasi hiyo, Joyce Msuya alikuwa Naibu Mkurugenzi wa shirika hilo Mei, 2018. Amewahi kufanya kazi kama Mshauri wa Benki ya Dunia kwa ukanda wa Asia Kusini na Pasifiki.

Msuya ni Mtaalamu wa Sayansi ya Maikrobailojia na kinga. Mama huyo wa watoto wawili ana uzeofu wa zaidi ya miaka 20 wa kufanya kazi kwenye mashirika ya kimataifa ikiwemo WB.

WABEBA nyama kwenye machinjio na mabucha watachukuliwa hatua za kisheria ...

foto
Mwandishi: Janeth Mesomapya

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi