loader
Drogba astaafu rasmi soka

Drogba astaafu rasmi soka

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Chelsea na Ivory Coast Didier Drogba ametangaza rasmi kustaafu soka.

Drogba mwenye umri wa miaka 40 amefunga mabao 164 katika mechi 381 kwenye vipindi viwili alivyoichezea Chelsea, huku akiisaidia klabu hiyo kushinda taji la Ligi Kuu ya England mara nne na Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2012.

Pia ameshinda kombe la FA mara na kombe la Ligi mara tatu wakati akikipiga kwenye klabu hiyo yenye maskani yake katika jiji la London.

Drogba kwa kipindi cha karibuni amekuwa akiichezea klabu ya Phoenix Rising ya Ligi Daraja la Pili ya Marekani ambapo pia akiwa mmiliki mwenza wa klabu hiyo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/d79cb8ccf3918060d9a44d6155a2ace9.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi